Septemba 30, 2015 Jijini Mbeya:
Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali linalotoa misaada katika jamii lijulikanalo kama Hassan Maajar Trust (HMT) wametoa mchango wa madawati 700 yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 49 kwenye shule za msingi 32 katika wilaya ya Rungwe, Mbozi na wilaya ya Mbeya Mjini.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika moja ya shule jijini Mbeya, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema: “ mchango huu ni sambamba na dhamira ya kampuni ya kuunga mkono mipango ya kijamii kupitia wigo wake wa kushirikisha jamii”.
“Kupitia mchango huu, kampuni ya Tigo inawajibika katika kutengeneza viongozi wa baadaye wakiwamo madaktari, wahandisi na wataalamu wengine wa nchi hii, "alisema Gutierrez.
Alisema, katika miezi ya hivi karibuni kampuni ilitoa mchango kama huo wa madawati katika mikoa ya Iringa na Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya dola za Marekani 50,000 kwa serikali, ahadi ambayo kampuni ya Tigo ilitoa mwaka jana ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule za umma nchini.
Makabidhiano yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye alisema madawati hayo700 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika wilaya hizo tatu, akitoa wito kwa wadau wengine wenye mapenzi mema kujitolea na kujiunga kwenye jitihada za kukabiliana na sehemu iliyobaki ya uhaba wa madawati mkoani humo.
Picha na habari kwa hisani ya http://bongodailyupdates.blogspot.com/
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.