ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 1, 2015

PAPA FRANCIS AKUTANA NA KARANI ALIYEKATAA NDOA ZA JINSIA MOJA.

Papa Francis                                                                                   Kim Davis

CHANZO: BBC SWAHILI
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameripotiwa kukutana na Kim Daviz karani wa Kentucky ambaye alifungwa jela kwa kukataa kutoa leseni za ndoa za wapenzi wa jinsia moja,wakati wa ziara yake huko Marekani.
Wakili wa bi, Davis amesema alikuwa na mkutano wa faragha uliochukua dakika 15 na papa Francis huko Vatican mjini Washington.
Hata hivyo msemaji wa Vatican Frederico Lombardi amesema kuwa hakatai kwamba mkutano ulifanyika. Bi Davis anapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja na anahoji kwamba dini yake haimruhusu kutoa vibali kama hivyo.
Alihudumia kifungo cha siku sita mahakamani mapema mwezi huu baada ya kukiuka agizo la mahakama ya kijimbo kutoa leseni hizo kwa wanandoa wa jinsia moja huko Rowan mjini Kentucky.
 
Mat Stavers,ambaye ndio wakili wa Davis amekiambia chombo cha habari cha CBS kwamba bi Davis na mumewe walikuwa wamealikwa kukutana na papa Francis kufuatia msimamo wake uliotangazwa na vyombo vya habari.
''Papa Francis alimshukuru kwa ujasiri wake na kumwambia aendelee na mwenendo huo'', alisema Bwana Stavers.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.