MTOTO Julias Makoye (5) mkazi wa Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga amenusurika kifo mara baada ya kuchomwa moto na Edina Peter 20, kwa tuhuma ya kuiba simu na rimoti ya televisheni.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo limetokea juzi ambapo Edina amefanya ukatili kwa mtoto Julias kwa kumwagia mafuta ya petrol mwili mzima na kisha kumchoma moto uliomsababishia majeraha mwilini.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwendakulima kati Abrahamani Dulla, amesema kuwa mara baada ya Edina kutekeleza tukio hilo walimchukua mtoto Julias bila kuwapa taarifa wazazi wake na kumpeleka katika Zahanati ya Nyakato mjini Kahama.
Mama mzazi wa mtoto huyo Ndalo Manyanda amesema mwanaye alikuwa anacheza katika nyumba ya jirani na ghafla alipokea taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanaye amechomwa moto kwa tuhuma ya kuiba simu na rimoti ya televisheni.
Amesema kuwa hali ya mtoto wake inaendelea vizuri mara baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama huku akitoa rai kwa wasamaria wema kumsaidi fedha ili mwanaye apatiwe matibabu zaidi.
Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na bado linaendelea kuwashikilia Chalya Charles 30 na mkewe Edina aliyedaiwa kufanya tukio hilo ili hatua za kisheria zipate kuchukuliwa dhidi yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.