ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 6, 2015

MAMA SAMIA SULUHU: Wanaohujumu Wakulima Tutawashughulikia.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Kata ya Mabama, Jimbo la Sikonge Tabora.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwapongeza mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sikonge, George Kakunda na aliyekuwa mpinzani wake katika kura za maoni, Said Nkumba (kukia) baada ya kumaliza tofauti zao na kuunda timu ya ushindi wa CCM.
Wagombea nafasi ya udiwani kupitia CCM Sikonge wakiwa katika mkutano wa hadhara jimboni humo.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya viongozi na makada wa CCM baada ya kuwasili Jimbo la Urambo Magharibi alipofanya mkutano wa hadhara.
Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Daudi Nteminyanda akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM leo, ambapo alikiponda chama cha Chadema.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Urambo Magharibi, Magreth Sitta akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimboni humo Mkoa wa Tabora jana.
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wenye vizibau wakiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za CCM jana.
Kundi la wasanii wa Bongo Movie makada wa CCM wakiwaburudisha wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Urambo Mashariki Wilaya ya Kaliua jana.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akiwa meza kuu katika mkutano wa kampeni wa CCM jana katika Kata ya Maboma.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan (katikati) akisaini kitabu cha wageni katika mkutano wa hadhara kampeni za CCM Jimbo la Tabora Kaskazini. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Hassan Wakasubi na kushoto ni mgombea ubunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Juma Kapuya. Mgombea ubunge wa Jimbo la Sikonge, George Kakunda akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Kata ya Mabama, Mkoa wa Tabora leo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Sikonge, George Kakunda akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Kata ya Mabama, Mkoa wa Tabora jana.

  MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan amesema endapo chama chake kitafanikiwa kushinda na kuunda Serikali kitahakikisha vyama vyote vya ushirika vya wakulima vinaangaliwa upya ili kuhakikisha vinawasaidia wakulima. 

Alisema wapo baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika ambao wanavitumia vibaya vyama vya ushirika na kuwanufaisha zaidi wao zaidi ya wakulima jambo ambalo limekuwa halina manufaa kwao. "...Tutaviangalia upya vyama vyote vya ushirika ili kuhakikisha tunaweka viongozi wenye utashi wanaoweza kuwanufaisha wakulima, maana wapo baadhi ya watu ambao wanajifanya mungu watu...wanataka wao waabudiwe hili halikubaliki hata kidogo," alisema mgombea mwenza. 

Mama Samia Suluhu alisema wamepanga kuiongezea uwezo taasisi iliyoanzishwa kwa ajili ya kushughulikia kero anuai za walimu ili iweze kuangalia masuala kama viwango vya mishahara ya walimu, upandishaji madaraja na vyeo vya walimu pamoja na maslahi mengine ya wafanyakazi. 

Alisema Serikali ya CCM itahakikisha maslahi ya wakulima na wafanyakazi yanaangaliwa kwa karibu kupitia taasisi maalumu ili kuchochea ufanisi na uwajibikaji kazini. Alisema ni jambo la kushangaza kuona wakulima wanalima mazao yao na baadaye kulipwa kwa taabu huku wakiwa wametumia gharama zao. 

Kwa upande wake aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Daudi Nteminyanda aliwaomba wananchi kukinyima kura chama hicho kwani hakina viongozi waadilifu zaidi ya viongozi maslahi. 

Alisema viongozi wa CHADEMA ni vigeugeu ambao hawapaswi kupewa uongozi wa nchi kwa kile kuwakumbatia watu kiliokuwa kikuwaita mafisadi hapo awali lakini leo kimewapa nyazifa za juu. 

Kiongozi huyo wa Chadema ambaye alishinda kura za maoini katika nafasi yake na baadaye kukatwa nafasi yake kisha kupewa aliyekuwa kada wa CCM, Josef Kidaha aliyehamia Chadema kwa sasa amekikimbia chama cha Chadema na kujiunga na CCM, huku akikinadi ndiyo chama pekee shupavu kitakachoreta maendeleo. 

Mama Samia Suluhu leo amemaliza ziara ya kampeni Mkoani Tabora baada ya kufanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Urambo Magharibi, Urambo Mashariki, Tabora Kaskazini-Uyui, na Jimbo la Sikonge. Kesho anaelekea Mkoa wa Kigoma kuendelea na ziara yake ya kampeni kunadi ilani ya CCM. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.