ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 28, 2015

PICHA NA STORY AIRTEL FURSA PLS MKUUU PICT 2: Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi akisalimiana na Innocent Kipondya, kijana aliyewezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa Katika kijiji cha Mabanda wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. Huku wakishuhudiwa na ndugu wa Innocent na wafanyakazi wa Airtel mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya generator, pampu ya maji na vifaa vingine vya Kilimo.

 PICT 3: Wafanyakazi wa Airtel wakibeba zawadi kwa ajili ya kijana Innocent Kipondya (hayupo pichani) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” uliozinduliwa miezi miwili iliyopita jiji Dar Es Salaam.

 PICT 4: Innocent Kipondya (kushoto) akipokea zawadi ya generator, pampu ya kumwagilia maji na vifaa vingine vya Kilimo kutoka Airtel mara baada ya kuibuka miongoni mwa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” uliozinduliwa miezi miwili iliyopita jiji Dar Es Salaam.

 Airtel Fursa Yamuwezesha Kijana Mwingine Kutoka Mkoa Wa Mwanza. Katika kijiji cha Mabanda wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imemuwezesha mkulima mdogo Innocent Kipondya, anayeendesha kilimo cha mbogamboga kwa kumkabidhi zana bora za Kilimo kwa ajili ya kuendeleza biashara yake.

Innocent alimaliza elimu ya sekondari, kidato cha nne mnamo mwaka 2011, hakufaulu kuendelea na masomo , alitamania sana kufanyabiashara ya Kilimo lakina hakuwa na mtaji, alifikiri kwenda mjini kutafuta kazi lakini hakujua pa kuanzia ndipo alipoamua kujikita kwenye kilimo cha biashara kijijini kwao. 

 Airtel Kupitia mradi wake wa Airtel Fursa, uliona juhudi za kijana Innocent za kutaka kujikomboa na maisha na kuepukana na vishawishi vinavyowakumba vijana wengi hapa nchini hivyo kuamua kumkabidhi zana zilizobora zitakazomuinua katiaka biashara yake. 

 Wakati wa makabidhiano ya vifaa vya hivyo, Meneja wa Airtel wa huduma kwa jamii, Hawa Bayumi, alisema “leo hii tunamkabidhi Innocent vifaa hivi kutokana na changamoto anazokumbana nazo katika kuendeleza biashara yake. 

Airtel, kupitia mradi wake wa Airtel Fursa tumeona ni muhumu kumuwezesha ili aweze kukuza biashara yake na kuongeza thamani kwenye mazao yake na kuyauza kwa bei nzuri”. Hawa aliongeza kwa kusema, “Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye lengo la kuhamasisha vijana, kuwapa fursa ya kujiendeleza kibiashara na kuwapa ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao . 

Mradi huu unalenga kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 waweze kujikwamua kiuchumi na unalenga kuwasaidia wale vijana wanaoonyesha kujituma kiuchumi. “Na huo sio mwisho wetu kwani Airtel Fursa bado inaendelea kuwawezesha vijana hapa nchini. 

Airtel inaona fahari kuwa sehemu ya jamii katika kuisaidia serikali kuwakwamua vijana kiuchumi”. Kwa upande wake Innocent aliwawashukuru Airtel kwa kusema, “nawashukuru sana Airtel kwani wameweza kubadili maisha yangu na familia yangu. 

Kwani kutokana na zana duni kwa wakulima wa mbogamboga vijijini ni aina nyingine ya vikwazo vinavyotukwamisha wakulima tusifikie malengo ya kupanua kilimo na kupata mazao mengi mashambani” “Mbali na zana duni, baadhi ya wakulima vijijini wanalima bila kufuata kanuni bora za kilimo na hivyo kujikuta tukipata mazao hafifu. 

Kutokana na elimu niliyopewa na Airtel ninaamini kabisa nitaweza kuboresha biashara yangu na kuwa mfanya biashara mkubwa hapa nchi na hata nje ya nchi.” “Ili kijana kama mimi aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. 

Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.