ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 28, 2015

CCM KATA YA KIRUMBA YATOA SARUJI MIFUKO 50 KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA SEKONDARI ZA KIRUMBA NA KABUHORO

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba, Abubakar Kweyamba (wa pili kutoka kushoto), akikabidhi saruji mifuko 25 kwa Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kabuhoro Kata ya Kabuhoro, Nhyanya Ndaji, juzi kwa ajili kusaidia ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara uliochelewa kuanza kutokana na changamoto ya ulipaji fidia wa maeneo yanayozunguka shule hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba, Abubakar Kweyamba (katikati), akifurahia baada kukabidhi saruji mifuko 25 na kupongezwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kirumba Kata ya Kirumba, Nhyanya Ndaji, juzi kwa ajili kusaidia ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara uliochelewa kuanza kutokana na changamoto ya ulipaji fidia wa maeneo yanayozunguka shule hiyo. Picha Na Peter Fabian. 
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba, Abubakar Kweyamba, wa pili kutoka kulia akipewa maelezo ya ujenzi wa msingi wa majengo ya vyumba vitatu vya maabara ya sekondari ya Kirumba na Mtendaji wa Kata ya Kirumba, Abraham Kapama (kushoto) baada ya kukabidhi mifuko 25 ya saruji kuchangia ujenzi huo. 
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba, Abubakar Kweyamba (kulia) akishiriki kujenga msingi wa vyumba vitatu vya maabara sekondari ya Kirumba juzi baada ya kukabidhi saruji mifuko 25 kati ya mifuko 50 alizotoa kwa sekondari mbili ikiwemo ya Kabuhoro kusaidia ujenzi huo na kushoto ni Mkuu wa sekondari hiyo, Margareth  Mnyone, akisaidia kumpatia jiwe kwa ajili ya ujenzi huo. 
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba, Abubakar Kweyamba (kulia) akishiriki kujenga msingi wa vyumba vitatu vya maabara sekondari ya Kirumba juzi baada ya kukabidhi saruji mifuko 25 kati ya mifuko 50 alizotoa kwa sekondari mbili ikiwemo ya Kabuhoro kusaidia ujenzi huo na kushoto ni Mkuu wa sekondari hiyo, Margareth  Mnyone, akisaidia kumpatia jiwe kwa ajili ya ujenzi huo.

NA PETER FABIAN, MWANZA.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kirumba, kimepiga tafu kwa kutoa saruji mifuko 50 kusaidia ujenzi wa Maabara katika shule za sekondari za Kabuhoro na Kirumba zilizopo Kata ya Kirumba wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Akikabidhi saruji hiyo juzi, Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo, Abubakar Kweyamba, alisema kuwa hatua hiyo inatokana na kuchelewa kuanza utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, kuwa kila shule ya sekondari ya Kata kukamilisha ujenzi wa maabara tatu za Kemia, Baioloji na Fizikia ifikapo mwisho wa Mwezi Juni mwaka huu. 

Kweyamba alieleza kuwa kutokana na changamoto ya kulipa fidia maeneo yanayozunguka shele hizo za sekondari kulisababisha ujenzi kushindwa kuanza kwa wakati na baada ya kumalizika kwa suala hilo, CCM imechukua hatua za kusaidia ujenzi huo na kuhamasisha wananchi kuchangia ili kutekeleza agizo hilo la Rais Kikwete.

“Tunaunga mkono kauli ya Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa juu ya utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 hadi 2015 kwa vitendo, lakini kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu ya nadhalia na vitendo katika msingi wa kuwajengea uelewa zaidi wa taaluma wanazosomea,”alisisitiza.

Kweyamba akikabidhi saruji mifuko 25 katika kila sekondari ya Kirumba, aliwataka walimu na wanafunzi kutoendekeza porojo na ushabiki wa kisiasa na badala yake watekeleze kutoa taaluma inayokusudiwa kwa wanafunzi na wanafunzi pia wawe na jukumu moja tu la kusoma ili kuwa na ufahamu zaidi wakizingatia kuwa ndo suala muhimu zaidi kwao.

“Walimu jiepusheni na kujishughulisha na masuala ya kisiasa mkiwa shuleni hususani ushabiki na kuanza kuhubili wanafunzi kujiunga na vyama vya siasa wakati wa masomo, kazi yenu ni kuwapa maarifa, siasa tuachieni sisi na wanafunzi kazi yenu moja tu kusoma kwa bidii kwa nadharia na vitendo ili kuwa wataalamu wazuri badae mtakaokuwa na nyadhifa kubwa badae na kulisaidia taifa kupiga hatua za maendeleo,”alisisitiza.

Mwenyekiti huyo pia alizitaka Bodi za shule hizo kushirikiana na wazazi na wadau  ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kuchangia ujenzi kwa kutoa vifaa na fedha na kufanya kazi iliyokusudiwa ili kujenga imani kwao na kusaidia ujenzi huo kukamilika kwa haraka na walimu na wanafunzi kufundisha na kupata elimu bora kwenye majengo yaliyo na ubora zaidi.
  
Naye Mkuu wa Sekondari ya Kabuhoro, Nhyanya Ndaki, alisema kuwa pamoja na msaada huo bado inahitaji mifuko mingine 100 ya saruji, mabati bando sita, misumari na fedha kwa ajili ya kulipia mafundi ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kama ilivyoagizwa na serikali chini ya Rais Dkt. Kikwete.

Kwa upande wake Mkuu wa Sekondari ya Kirumba, Margareth Mnyone, alisema kuwa changamoto ya ulipaji fidia imesababisha kuanza ujenzi wa msingi wa vyumba vitatu Mei 27 mwaka huu, lakini pia upatikanaji wa maji kwa ajili ya ujenzi, vifaa na kuwepo poropoganda za wanasiasa kuhamasisha jamii kutochangia vifaa, fedha na nguvu kazi jambo ambalo lichachukua muda kukamilisha ujezi haraka.

“Tukishukuru Chama hiki kutambua hili na kutusaidia saruji mifuko 25 ili kuendelea na ujenzi, pamoja na kuchelewa tukipata kuungwa mkono na wazazi na wadau wengine tunaweza tukafikia malengo na kukamilisha ujenzi ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa, lakini niwaombe viongozi wa Bodi wafanye jitihada ili kuweza kushirikisha wenyeviti wa mitaa kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchangia,”alisema.

Akitoa shukurani kwa msaada huo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ibanda ya Juu, Ephrahim Nkingwa (Chadema) aliupongeza uongozi wa CCM Kata ya Kirumba kutoa msaada huo kutokana na kulenga kuleta maendeleo na uboreshaji wa mazingira ya utolewaji wa elimu kwa wanafunzi jambo ambalo linapaswa kuigwa na vyama vingine kikiwemo Chama chake cha CHADEMA kwa kusema kuwa maendeleo hayana Itkadi za Chama.

Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Kirumba, Daniel Kahungu (CHADEMA) aliyekuwepo katika eneo la Sekondari ya Kabuhoro alitoweka na kushindwa kuvumilia kushirikiana  na Mtendaji wa Kata ya Kirumba, Abraham Kapama, walimu na baadhi ya watendaji wa mitaa na wenyeviti wa serikali za mitaa yote 12 ya Kata hiyo waliokuwepo kupokea na kuangalia ujenzi unavyoendelea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.