ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 28, 2015

WACHEZAJI WAPATAO 136 WACHAGULIWA KUUNDA TIMU YA MKOA WA PWANI MASHINDANO YA UMISSETA

Picha matukio ya UMISSETA kutoka maktaba.
NA VICTOR MASANGU, PWANI  
 
JUMLA ya wachezaji wapatao 136 wanaoshiriki katika  michezo ya aina  mbali mbali wamechaguliwa kuunda kikosi cha  timu ya Mkoa wa Pwani ambacho kinatarajiwa kwenda kushiriki katika michuano ya Umoja wa michezo na sanaa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) katika ngazi ya kanda ya mashariki  Mkoani Morogoro.
  
Akizungumza na mwandihi wa habari hizi kuhuisiana na kuundwa kwa kikosi hicho cha wachezaji Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani  Grace Buleta alisema kwamba kwa sasa mipango yote inaendelea vizuri kwa ajili ya kujiweka sawa na safari ya kuelekea mjini Morogoro ambapo mashindano hayo yatafanyika chuo cha ualimu mwezi ujao.
 
Grace alisema kwamba kuundwa kwa kikosi hicho cha timu ya Mkoa wa Pwani kimewashirikisha walimu na wataalamu wa michezo ya aina mbali mbali ambapo wamezingatia vigezo vingi ikiwemo suala la nidhamu kwa wachezaji uwezo walionao pamoja na mambo muhimu ambayo ni yamsingi katika medani ya michezo.
 
“Kwa sasa tulikuwa katika viwanja vya shule ya msingi Filbert bayi kwa muda wa siku tatu hivi na nia na madhumuni ya kukutana hapo ni kufanya uchaguzi wa wachezaji 136 ambapo zoezi ili tunashukuru tumelikamisha salama kwa kupata vijana hao ambao ndio watauwakilisha Mkoa wetu wa Pwani katika ngazi inayofuata.,”alisema Grace.
 
Aidha Afisa huyo alisema kwamba zoezi la kuunda kikosi hicho pia limezishirikisha timu mbali mbali kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo, Mkuranga, Rufiji, Bagamoyo, Kibaha Mji, Kisarawe, Mfafia pamoja na Kibaha vijinni lengo ikiwa ni kupata kikosi ambacho ni bora.
 
Pia alibainsiha kwamba baada ya kukamilisha zoezi hilo wachezaji wataingia kambini rasmi kwa muda wa siku tatu katika viwanja vya shule ya msingi Firbert bayi na baada hapo wataelekea safari ya kwenda Mkoani Morogoro kwa ajili ya  kumenyana na timu hiyo ambapo maara baada ya hapo wataunda timu moja ya kanda ya mashariki ambayo itakwenda kushiriki katika michuano ya Taifa ambayo kwa mwak huu yamepangwa kufanyika Jijini Mwanza mwezi ujao.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule za msingi na sekondari za  Filbert bayi Anna Bayi ambaye ni mdau mkubwa wa michezo alisema a kwamba licha ya wachezaji hao kuweka kambi  katika shuke yake lakini ndoto yake kubwa ni kuhakikisha anaboresha viwanja vya michezo vya aina yote ili kuweza kuwapa fursa vijana wadogo  ambao wataweza kuleta mapinduzi katika medani ya michezo.
 
Mama Bayi alisema kwamba anatambua katika Mkoa wa Pwani kunachangamoto kubwa ya viwanja hivyo kwa upande wake atakikita zaidi kulivalia njuga suala hilo ambalo limeonekana kuwa ni tatizo sugu kwani linasababisha kuwapa fursa wachezaji wenye vipaji kutoonyesha uwezo wao kutokana na uhaba huo wa viwanja.
 
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kwamba wadau wa Mkoa wa Pwani wanapaswa kushirikiana kwa hali na mali katika kukuza maendeleo ya michezo ya aina zote ili kuweza kuwapata wachezaji wazuri ambao watakuwa ni mkombozi wa Taifa katika siku za usoni kwani ana imani kuwa vijana wadogo  wakifundishwa mapema wataweza kuleta mapinduzi makubwa katika Taifa la Tanzania na kupata timu nzuri.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.