Kutanda kwa mimea hiyo katika eneo lenye ukubwa wa takribani hekari 4 kulisababisha vivuko vya Mv Misungwi na Mv Sengerema kushindwa kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwa takriban siku tatu mfululizo baada ya kukosa eneo la kutia nanga katika eneo la Kigongo.
Wananchi waliojitolea wakihangaika kuyakata magugu maji na kuyaondosha kwa kutumia nyenzo hafifi na vifaa duni katika eneo la Kigongo jitihada huku ukosefu wa vifaa pamoja na wataalamu ukiendelea kuwa kikwazo.
Ferdinand Mshamo ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA mkoa wa Mwanza (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)
Katika eneo la Kigongo jitihada za kuondoa mimea hiyo aina ya matende zinaendelea huku zikikwamishwa na ukosefu wa vifaa pamoja na wataalamu.
Zaidi ya magari 200 ya mizigo yamekuwa katika eneo la Kigongo na Busisi na kuleta athari kubwa kwa wananchi, wafanyabiashara na wasaka huduma. Wananchi pamoja na madereva nilio kutana nao eneo la Kigongo Ferry wanazungumzia changamoto walizokutana nazo mara baada ya kadhia hiyo kujitokeza. (BOFYA PLAY KUWASIKILIZA )
Magugu maji ni tatizo katika ziwa Victoria, ambapo hivi karibuni ongezeko lake linatajwa kuwa ni kutokana na uchafuzi wa mazingira katika mito inayoingiza maji yake ziwani Victoria.
Zaidi ya magari 200 ya mizigo yamekwama katika eneo la Kigongo na Busisi na kuleta athari kubwa kwa wananchi, wafanyabiashara na wasaka huduma.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.