ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 16, 2015

KAMATI YA AMANI MKOA WA MWANZA YA VIONGOZI WA DINI YAWAALIKA WANANCHI KUHUDHULIA KONGAMANO LA KIPEKEE LA KWANZA LA AMANI

Baba Askofu Charles Sekelwa (mwenye miwani) ambae ni Mwenyeki Mwenza wa Kamati, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Kongamano la Amani.
Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikiristo Mkoani Mwanza, imetoa rai kwa Wananchi Mkoani Mwanza sanjari na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika kuhudhuria Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika Mwishoni Mwa Mwezi huu Mkoani Mwanza.

Askofu Sekelwa alibainisha kwamba kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 28 ya Mwezi huu katika Uwanja wa Furaisha kuanzia majira ya Saa mbili asubuhi hadi saa Saba Mchana, huku akiongeza kuwa Kongamano hilo litahitimishwa katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kutakuwa na mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Dini zote mbili za Kiislamu na Kikiristo kuanzia majira ya saa tisa mchana.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Kwanini mmeamua sasa kuja na wazo la Kongamano la Amani na si wakati Mwingine? BOFYA PLAY KUSIKILIZA JIBU.

Baba Askofu Zenobius Isaya (Katibu) akijibu moja ya maswali.
Mikoa ya Kanda ya ziwa imekuwa ikihusishwa na matukio mengi ua ukiukwaji wa haki za binadamu kama Mauaji ya Vikongwe, Ukataji viungo sanjari na mauaji ya watu wenye Albinism na mambo kadha wa kadha, pamoja na Lengo kuu mliloweka nini kimewasukuma hatimaye mkaja na wazo la Kongamano lenye kuwahusisha Waislamu na Wakristu kwa wakati mmoja? BOFYA PLAY KUSIKILIZA JIBU.


Wanahabari wakinasa habari....
Sheikh Mohamed Salum Balla (Katibu), akijibu swalikuhusu mahakama ya Kadhi.
Nini msimamo wa Mashekhe wa mkoa wa Mwanza kuhusu Mahakama ya Kadhi? BOFYA PLAY KUSIKILIZA JIBU.

Wanahabari waliokuwa katika Mkutano baina yao na Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza wakati Kamati hio ikitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 28.02.2015 katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza
Sheikh Hassan Kabeke (Mwenyekiti). akijibu swali lililoulizwa hapa chini.
Nchi sasa inaelekea katika masuala makubwa mazito, Kwanza suala la Kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa, Pili Uchaguzi Mkuu. Nini kauli yenu juu ya haya yanayogusa eneo nyeti la maisha ya Watanzania? BOFYA PLAY KUSIKILIZA JIBU.

Wanahabari waliokuwa katika Mkutano baina yao na Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza wakati Kamati hio ikitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 28.02.2015 katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza.
Lengo la Kongamano hilo la Amani ni kutoa elimu ya Umuhimu wa Amani na Mahusiano kwa Watu na rika zote ili kudumisha amani na utulivu, ambapo alibainisha kwamba elimu hiyo itatolewa na Wanazuoni mbalimbali kutoka dini zote mbili za Kiislamu na Kikristo.
Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Kamati hiyo kutoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 28.02.2015 katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza, Kongamano ambalo litahitimishwa tarehe hiyo hiyo katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kutakuwa na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Viongozi wa Serikali pamoja na viongozi dini zote mbili za Kikiristo na Kiislamu.
Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo Mkoani Mwanza iliundwa tangu mwaka 2013 ikiwa na Wajumbe 20 kwa maana ya Maaskofu 10 kutoka Mabaraza yote ya Kikristo nchini pamoja na Masheikh 10 kutoka Baraza la Bakwata sanjari na Taasisi mbalimbali za Kiislamu.

Kaulimbiu ya Kongamano hilo la Amani ni 'Tunaishi Pamoja, Tunakula Pamoja, Tunacheza Pamoja katika Nchi Moja'

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.