Ukaguzi wa vituo vya Afya, picha toka maktaba yetu. |
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza kupitia Idara ya Afya itaendeleza msako kwa watu ambao ni wafanyabiashara wanaomiliki maduka bubu ya kuuza dawa za binadamu kinyume na taratibu na sheria Jiji Mwanza.
Mfamasia wa Halmashauri ya Jiji, Edward Magelewanya, alieleza kuwa, kikosi kazi kitafanya zoezi la kukagua maduka ya kuuza dawa za binadamu, sambamba na msako kwa wamiliki wa maduka yasiyokuwa na leseni, kibali cha Baraza la Famasi Tanzania, usajili wa majengo ya kutolea huduma na ubora wake.
Magelewanya alisema kuwa kikosi kazi hio kinachounndwa na kushirikisha Maafisa kutoka Ofisi nyigine ikiwemo ya Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) za Nyamagana na Ilemela, Idara ya Afya Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilemela Maafisa Biashara wa Jiji na Manispaa ya Ilemela na Wadendaji wa Kata husika.
Aliongeza kuwa kikosi hicho pia kitashirikisha Taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Mkoa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakati wa utekelezaji wa zoezi endelevu la ukaguzi maalumu unaoambatana na msako wa wamiliki wa maduka binafsi ya dawa wanaouza dawa za Serikali zenye alama ya Government of Tanzania (GOT).
“Tutawakamata wale wote na kuwafikisha Mahakamani ili kuchukuliwa hatua za kisheria watakaobainika kutofuata taratibu, kanuni, kutokuwa na leseni, vibali, usajili wa majengo na ubora wake, kufatilia ili kuona kama wataalamu wanaotoa huduma za dawa kwa walaji kama wana vyeti vinavyokidhi vigezo na sifa ya kufanya kazi inayotambuliwa na Baraza la Famasi.
Magelewanya kumekuwepo na taarifa za baadhi ya wamiliki wa maduka bubu tuliowafungia kwa kukosa sifa lakini wamekuwa wakifanya biashara ya kuuza nyakati za saa 1 usiku kwa kudhani hatutaweza kuwafuata, sasa tumedhamilia kazi hii itafanyika nyakati zote za mchana na usiku lengo ni kuhakikisha taratibu zinafuatwa na si kumwonea mtu bali kwa utekelezaji wa sheria.
“Utekelezaji wa zoezi hili pia umelenga kuchukua hatua stahiki na kuangalia Nyaraka muhimu za utendaji kazi katika maduka hayo ya watu binafsi na kupitia vitabu vya rejea ikiwemo kufatilia kwa umakini majengo yanayotoa huduma ya jumla kama yanauza dawa kwa wamiliki wa maduka yaliyosajiliwa pia kama yanauza rejareja kwa walaji bila kufuata taratibu zilizopo,”alisisitiza.
Wito kwa wananchi, tunaomba kutupatia ushirikiano pia kutupatia taarifa za siri zitakazowezesha kuwakamata wamiliki wa maduka binafsi wanaouza dawa za serikali kinyume na taratibu na sheria pamoja na wanaotoa huduma zilizo kinyume ikiwemo kuchoma sindano wateja wao, kuwalaza kwa muda na wanaofanya biashara wakati wameisha fungiwa maduka yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.