ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 6, 2014

WAHINDI WASHEREHEKEA SIKU YA ASHURA NA KUTAKA WAUMINI WA KISLAMU KUSOMA NA KUIELEWA QURAN

 NA PETER FABIAN,
 WA GSENGO BLOG,
 MWANZA.

WAUMINI wa Kislamu nchini wametakiwa kusoma zaidi Quran na vitabu vingine vinavyoeleza misngi imara ya dhebu hilo na kuyaelewa yaliyomo badala ya kukimbilia kuhubili mambo ya kidunia na kiutawala ambayo ni kinyume na inavyoelekezwa.

Kauli hiyo imetolewa juzi na kiongozi wa Msikiti wa Dhehebu la Wahidi ambao ni waislam, Mohamed Moridina wakati wa kilele cha kuazimisha sherehe ya “ASHURA” iliyoambatana na mafunzo na maandamano ya kuzunguka katika barabara za mtaa wa Libert, Nyerere, Nkuruma na Jaffaries na kisha kuishia mskiti wa Shia Ithna Ashery Asghery uliopo mtaa wa Nkomo jijini hapa.

Pia kushiriki kwao katika  kusoma yale yaliyosimamiwa na kiongozi wao Imam Hussein jinsi ya kushinda dhulma hali ukiwa unadhulumiwa jambo ambalo likifanyika litasaidia watoto wadogo kutambua misingi na maandiko hayo kwa kuwapeleka kwenye nyumba za ibada badala ya kuwaacha majubani wakiangalia Tv na kufanya mambo ambayo yatasababisha wao kupotoka.

Moridna alisema kwamba kutokana na waumini wengi kujihusisha na vitendo ambavyo haviendani na maandiko ya vitabu vya dini vimesababisha kuwepo vitendo viovu ikiwa ni pamoja na ubakaji, kutumia dawa za kulevya, uchochezi na hata kutumia uhuru wa kukejeri baadhi ya madhehebu ya dini nyingine.
 Kiongozi huyo alisema kwamba iwapo waumini wa kislamu watazingatia kusoma zaidi vitabu vya dhehebu hilo na kuzingatia misingi imara ili kuwawezesha kuwa waumini wanaotambua mambo ya kidini na utawala wa kidunia badala ya kuchanganya na kutumia vivuli vya dini kufanya maovu.

“Tunatakiwa kuwa na ujasili wa kutetea haki kama Imam Hussein, Marehemu Rais Nerson Mandela alipokuwa alipokuwa amefungwa gerezani  na  vingozi wa serikali ya Makaburu baada ya kuwa jela miaka 20 kwa kukataa kutii amri ya makaburu hao siku moja alikumbuka yaliyofanya na Imam Hussein,”alisema.

Aliongeza kuwa Mandela ghafla alipata kusoma na kukumbuka maneno ya Imam Hussein katika harakati za Kerbala na kumpa nguvu ya kupambana na makaburu ili haki ya kuwa huru ipatikane ikiwa ni pamoja na kulikomboa Taifa la Afrika kusini jambo alilifanikiwa.

Aidha ameipongeza serikali kwa kusimamia vyema haki na taratibu kwa kutoa uhuru wa kuabudu kwa madhehebu ya dini mbalimbali pamoja na kushirikiana na madhehebu hayo kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwa nguzo ya taifa hili.

“Serikali haina ubaguzi wa dini wala rangi hivyo ni vyema wananchi tukashirikiana na serikali kudumisha misingi hii ili taifa letu liendelee kuwa na amani na utulivu uliopo, na kukomesha tabia ya watu wachache wanaotaka kuivuruga kwa kisingizio cha dini,
Aliongeza kuwa ukiwepo kubaguana kikabila na rangi zetu ni jambo ambalo likiachwa kuwepo viashilia hivyo na bila kukemewa na viongozi wa dini, siasa na serikali litasababisha ufa na kuanza kutowekwa kwa amani iliyopo,”alisisitiza.

Wito wangu kwa waumini na wana jamii kushirikiana kupinga na kukomesha unyanyasaji wa aina yoyote unaofanywa na baadhi ya watu ambao hawataki kumwamini mungu na kurejea katika maandiko ya vitabu vya mungu na viongozi wengine wa serikali kutumia mamlaka yao kuwakandamiza wananchi.
Wauminiwa Msikiti wa Dhehebu la Wahidi ambao ni waislam, wakiwa katika maandamanoya kilele cha kuazimisha sherehe ya “ASHURA” wakiwa katika mtaa wa Nyerere jijini  Mwanza.
Maandamano ya kuzunguka katika barabara za mtaa wa Libert, Nyerere, Nkuruma na Jaffaries na kisha kuishia mskiti wa Shia Ithna Ashery Asghery uliopo mtaa wa Nkomo jijini hapa yakiendelea.
Akinamama na watoto nao walikuwa mstari wa mbele katika sherehe hizo.
Safu ya mbele katika maandamano ya kilele cha kuazimisha sherehe ya “ASHURA” iliyoambatana na mafunzo na maandamano ya kuzunguka katika barabara za mtaa wa Libert, Nyerere, Nkuruma na Jaffaries na kisha kuishia mskiti wa Shia Ithna Ashery Asghery uliopo mtaa wa Nkomo jijini hapa.
Viongozi mfano wa kuigwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.