ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 27, 2014

WATANZANIA WANG'ARA KATIKA ROCK CITY MARATHON 2014

Mtanzania Joseph Panga kutoka Manyara Tanzania akimalizia mbio za Rock City Marathon kwa kuinyakuwa nafasi ya kwanza akikimbia Kilomita 21 Wanaume kwa kutumia muda wa saa 1:02:36
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Sammy Nyakoye kutoka Kenya 1:02:39
Ya tatu ni Festus Talam kutoka Kenya 1:15:34.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani walijiandikisha kushiriki Rock City Marathon 2014 hivyo kutia hamasa katika kupendezesha na hapa wakipita katika njia tajwa ya ushiriki hii ni barabara ya Uhuru jijini Mwanza.
Wakubwa na wadogo walishiriki mbio za Kilomita mbili na tano.
Wadau mbalimbali wakishiriki Rock City Marathon jijini Mwanza.
Katikati ya jiji la Mwanza wafukuza upepo katika Rock City Marathon 2014 wakishughulika.
Kuelekea uwanja wa CCM Kirumba ni mmoja kati ya washiriki wa Rock City Marathon 2014  Kilomita 21 wanaume.
Mshindi wa kwanza Kilomita 2 watoto upande wa wasichana ni Irene Fidelin.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Jesca Amos huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Janeth Charles.
Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka (kulia nyuma) akiongoza picha ya pamoja na washindi wa Rock City Marathon Kilomita 5 wanawake Albino ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Irene Joseph, wa pili ni Asteria Abel huku nafasi ya tatu ikishikwa na Saidati Haji.
Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka (nyuma) akiongoza picha ya pamoja na watoto washindi upande wa wavulana mbio za Kilomita 2 ambapo Masumbuko Julias aliibuka mshindi, nafasi ya pili ikishikwa na Medadi Paulo, ya tatu ni Festo Daniel. 
Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka akifuatiwa na Meneja Kiongozi NSSF Mwanza Hamis Faki katika picha ya pamoja na washindi nafasi za juu Rock City Marathon Kilomita 5 wanaume Albino ambapo Paschal Charles kutoka Magu Mwanza aliibuka mshindi, nafasi ya pili ikikamatwa na Paschal Emmanuel naye kutoka Magu na ya tatu ikichukuliwa na George Joseph wa Ilemela Mwanza. 
Picha ya washindi na meza kuu ambapo mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 21 wanawake ni Mathalia Elisante kutoka Manyara Tanzania (kulia mwenye track suit ya njano) aliyetumia muda wa saa 1:14:25.
Wa pili niMary Naali Tz (katikati) aliyetumia muda wa saa 1:15:34
Wa tatu ni Adelina Audata Tz  (kushoto) aliyetumia muda wa saa 1:23:01
Mtanzania Joseph Panga kutoka Manyara Tanzania mshindi wa mbio za Rock City Marathon akikimbia Kilomita 21 Wanaume kwa kutumia muda wa saa 1:02:36 akionyesha kitita chake shilingi za Kitanzania milioni 1.5
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Sammy Nyakoye kutoka Kenya 1:02:39 zawadi ya shilingi za Kitanzania laki 9
Ya tatu ni Festus Talam kutoka Kenya 1:15:34. aliyepata zawadi ya shilingi laki 7 za Kitanzania.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza akihutubia umma uliojitokeza kushuhudia Rock City Marathon 2014 katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo moja kati ya ahadi aliyoweka amesema kuwa Ofisi yake itajipanga mwakani kuona ni jinsi gani inaweza kuboresha zaidi mashindano hayo ili yapate msisimko zaidi na hata kushuhudia baadhi ya wadau toka ofisi yake wakishiriki, kwani yanatumika kuitangaza wilaya yake.
Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka akizungumza na wadau waliohudhuria Rock City Marathon 2014 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mtanzania Joseph Panga kutoka Manyara Tanzania mshindi wa mbio za Rock City Marathon akizungumza na vyombo vya habari.
Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 21 wanawake ni Mathalia Elisante kutoka Manyara Tanzania  aliyetumia muda wa saa 1:14:25 akihojiwa na Star Tv.
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon Methew Kasonta pamoja na kuwashukuru wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha nchini na nje ya nchi kushiriki vyema kuyapamba mashindano hayo, vilevile ameyashukuru makampuni, taasisi na watu binafsi kwa kufanikisha Rock City marathon 2014.
Wadhamini wa Rock City Marathon 2014 ni pamoja na PPF, Air Tanzania, TSN Group, IPTL, Africa Barrick Gold...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.