MWANZA
Maandalizi kuelekea Michuano ya Kombe la Afrika Mashariki la Alliance yameanza kuchukuwa kasi jijini Mwanza.
Michuano hiyo itakayofanyika kwa mara ya kwanza nchini ikihusisha timu za shule mbalimbali za Alliance za Afrika Mashariki ambapo Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC Kongo zitashiriki, inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mnamo tarehe 26/09/2014 katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza, nazo fainali kuchezwa tarehe 27 na 28 mwezi huu Septemba 2014 katika viwanja vya Alliance Academy Mwanza vilivyo katika maboresho hivi sasa kwa hisani ya shirikisho la soka nchini TFF.
Kwa mujibu wa mratibu wa michuano hiyo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo cha elimu na michezo cha Alliance Academy ya jijini Mwanza, James Bwire amesema kuwa kila shule kutoka ukanda wa Afrika Mashariki imepewa nafasi ya kuingiza timu kwenye kategori tatu yaani umri chini ya miaka 13, 15 na 17 ambapo kila kategori itakuwa na Bingwa wake (BOFYA PLAY MSIKILIZE JAMES BWIRE)
Sehemu ya baadhi ya waandishi wa habari. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.