ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 30, 2014

"KIONGOZI ANAYE PINGA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA HATUFAI KWANI ANATAKA WANANCHI WAFE": UZINDUZI WA TIKA MANISPAA YA ILEMELA

"Kikao hiki kimeitishwa kwa kazi kubwa moja ya kujadili uanzishwaji wa TIKA katika Manispaa ya Ilemela, Hili suala ni nyeti na ningependa wote kwa pamoja mlijadili kwa kina na kwa mtazamo chanya kwani hakuna anayepingana nami kuwa gharama za matibabu ni kubwa ambazowananchi wetu wa kawaida ni ngumu kuzimudu" Alisema Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza wakati akizindua Semina ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, iliyofanyika katika ukumbi wa Monach Hotel, kujadili mustakbali wa Afya za watanzania.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda amewaasa Viongozi kuacha siasa za maneno na badala yake waihubiri kwa vitendo ikiwa pia na kuwahamasisha wananchi kuingia katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa huku wakihakikisha madawa na vifaa vyote vya tiba vinapatikana kwa wakati. 
Viongozi mbalimbali wa dini pia nao wameshiriki Semina hii. 
Kikao hiki kimeitishwa kwa kazi kubwa moja ya kujadili uanzishwaji wa TIKA katika Manispaa ya Ilemela, suala ambalo ni nyeti ambalo limejadiliwa kwa kina na kwa mtazamo chanya hasa ukizingatia kuwa gharama za matibabu ni kubwa ambazo wananchi wengi wa kawaida imekuwa vigumu kuzimudu. 
Sehemu ya kikao cha TIKA kilichoketi leo Monarch Hotel wilayani Ilemela mkoani Mwanza
Mfuko huu wa Afya ya Jamii (CHF) na TIKA ni msaada na mkombozi wa kweli wa afya za jamii lakini wananchi wengi bado hawajauelewa faida na manufaa yake. Mfuko huu umesaidia wengi mahali pengi nchini. Hivyo kimeketi kufikia maamuzi ambayo yataanzisha hamasa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa haraka iwezekanavyo.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya wilaya ya Ilemela wameshiriki kikao hiki muhimu. 
Ni asilimia 1.8 ya kaya zote mkoani Mwanza ndio walioko kwenye mpango huu lakini Manispaa ya Ilemela mpango huu bado haujaanza.
Kaimu mganga mkuu mkoa wa Mwanza Dr. Kengia akitoa shukurani za mkoa kwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuona umuhimu kwa wananchi kurahisishiwa huduma ya Afya kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, ambapo kupitia mpango huo gharama ni nafuu zaidi. 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Costantine Makala akizungumza na washiriki wa kikao cha kujadili Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, kilicho fanyika katika ukumbi wa Monach Hotel,
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wameshiriki kikao hiki.
JAMII imepewa majukumu mbalimbali yenye lengo la kuongeza ufanisi na kuogeza ubora wa huduma ikiwa ni pamoja na :-
- Kumiliki huduma za Afya
- Kushiriki katika kuweka mikakati
- Kuchagua wajumbe wa Bodi na Kamati
- Kuwajibika katika kulinda na kutunza mali na vifaa katika vituo vya huduma
- Kuchangia kwa hali na mali gharama za utoaji huduma za afya.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda akisisitiza jambo katika semina ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, iliyofanyika katika ukumbi wa Monach Hotel, kujadili mustakbali wa Afya za watanzania.
Wakuu wa Idara mbalimbali katika majeshi na sekta za kijamii nao wameshiriki semina hii.
Washiriki.
Iwapo vyombo hivi vitatimiza wajibu wake ipaswavyo wananchi watapata huduma bora wanazomudu kujigharamia na watatoa huduma watawezeshwa kutoa huduma bora na kwa ufanisi.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda akitoa mfano wa jinsi jamii yake ya watu wa Iramba ilivyoweza kuhamasishwa kupitia matoleo ya VCD  iliyo maalum kwajili ya kuifunza jamii mbinu mbalimbali za ujasiliamali ambapo  humo manufaa yake yatawawezesha kuchangia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Picha ya pamoja wakuu wa wilaya na wakuu wa sekta za Afya.
Picha ya pamoja meza kuu pamoja na viongozi wa dini.
Meza kuu na asasi za kiraia.
Meza kuu na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilemela.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.