Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akitambulisha viongozi na wageni kwenye kikao cha Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue jijini hapa. |
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Ndalo Kurwijila, akitoa taarifa ya mkoa kwa mgeni rasmi balozi Sefue. |
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jumanne Sagini akijibu hoja zilizo wasilishwa na watumishi katika kikao hicho. |
Watumishi kikaoni. |
Wakisikiliza kwa umakini. |
Wataalamu nao walihudhulia kikao hicho. |
Wajumbe wa sekretarieti ya mkoa wa Mwanza. |
Uwasilishaji hoja kikaoni. |
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa ya Sekou Toure akiwasilisha hoja za Idara ya Afya. |
Wadau wa kikao kwa umakiiiini. |
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hassan Hida akitoa neno la shukurani wakati wa kufunga kikao hicho. |
Picha ya pamoja. |
NA PETER FABIAN, MWANZA.
SERIKALI imewaagiza viongozi wa Mkoa na Jiji la
Mwanza kushirikiana na kuweka mipango na mikakati maalumu ya kuriboresha zaidii
Jiji hilo, ili kuwa Habu ya Ukanda wa nchi za Maziwa Makuu na Kituo cha
kimataifa cha Mikutano na Kibiashara nchini.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Omben Sefue wakati walipokutana na viongozi wa Mkoa wa Mwanza
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kupokea
taarifa fupi ya Mkoa huo kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani
humo.
Akizungumza katika Ofisi wa Mkuu wa Mkoa, Balozi
Sefue alisema kwamba uongozi huo kwa kushirikiana na ule wa Jiji la Mwanza
unatakiwa kuanza kuandaa mipango na mikakati ya kuriboresha na kulitanua zaidi
kuwa la kisasa nalenye sifa za kimataifa ili kuwa kivutio, kituo cha mikutano
kwa Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu barani Afrika na Senta ya biashara za
kimataifa.
“Ebua viongozi wa ngazi ya Mkoa kwa kushjirikiana na
wenzenu wa Jiji hili muanze kuweka mipango na mikakati na muanze kuitekeleza
kwa awamu, Jiji hili linakuwa kwa kasi kama mnavyoliona sasa na muanze
kulifikiria litakavyokuwa kwa miaka kumi hadi ishirini ijayo kwa kuriboresha na kulitanua zaidi, muweke mazingira
mazuri yatakayowavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,”alisema.
Balozi Sefue alisema kwamba viongozi wa Mkoa na Jiji
wawe na ubunifu wa mikakati itakayotekelezeka kirahisi ikiwa ni pamoja na
kuendelea kuboresha Miundombinu ya barabara zake, upatikanaji wa maji safi,
umeme, huduma za Afya kwa kuwa na Hospitali, Vituo vya afya, Vyuo, Shule na huduma Mawasiliano ya uhakika
na Uwanja wa Ndege wa kisasa, Usafirishaji wa majini na nchi kavu.
“Na uhakika hatutakuwa tunajadili tena habari ya
Jiji la Dar es salaam hata Nairobi kama ilivyo sasa na badala yake itakuwa
Mwanza, kama mtaweka vyema mipango na mikakati yenu na mkaitekeleza kwa awamu
kwa usitadi wa taratibu, kanuni na sheria za Mipago Miji basi Mwanza itakuwa
Habu na Senta ya Kimataifa kwa Mikutano na Biashara,” alisema.
Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikilo alimweleza
kiongozi huyo kuwa, tayari Halmashauri ya Jiji la Mwanza imetenga eneo la
uwekezaji katika Kata ya Buhongwa na eneo la Luchelele ambalo linasubilia
wananchi kulipwa fidia ili kupisha utekelezaji wa Mji mpya wa kisasa utakaokuwa
na huduma zote na kuwa limekuwa likiboresha maeneo ya Makazi na kuyauza ka
Taasisi, Mashirika, Mifuko ya Hifadhi za Jamii na wananchi.
Aidha Katibu Mkuu aliyeambatana na Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jumanne Sagini
na ujumbe wake, alimweleza Mhandisi Ndikilo kuwa tayari baadhi ya Wawekezaji
wakubwa wameanza kuvutiwa kuja kuwekeza Jiji la Mwanza kutoka mataifa ya China
na mataifa ya Bara la Ulaya kwa kuanza kuwasilisha maombi yao serikalini
kupitia Balozi zao na wengine kumueleza Rais Dkt. Jakaya Kikwete .
“Lakini nikupongezeni viongozi wote kwa kushirikiana
vyama na jamii na hasa mlivyoamua kutekeleza mkakati wenu wa kuwapanga katika utaratibu,
kanuni na sheria wafanyabiashara wadogo maarufu kwa “Machinga” hongereni sana
muendele kushirikiana na jamii, lakini inabidi viongozi wenzenu wa Mikoa yenye
Majiji na Wilaya zenye Manispaa waje kujifunza kwenu juu ya utaratibu
huu,”alisisitiza.
Aliongeza kuwa kutasaidia kumaliza mifarakano na
wamachinga hivyo viongozi wa Majiji ya Arusha, Tanga, Mbeya na hata Dar es
salamu na Manispaa zake za Ilala, Temeke na Kinondoni waje kujifunza na
kuchukua uzoefu wenu ili nawao waishirikishe jamii katika kutekeleza upangaji
wa Machinga hali itakayomaliza malalamiko wakati wa kuwaondosha na kuwapanga.
Balozi Sefue alitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa
jengo la kisasa la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kupatiwa taarifa fupi iliyosomwa
kwake na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) Ndalo Kurwijila lililokwama kukamilika kwa
muda mrefu sasa kutokana na kutekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa
fedha.
Ujenzi wa jengo hilo unaofanywa na Mkandarasi
Kampuni ya CEF Ltd ya jijini Mwanza tangu mwaka 2008 umeshindwa kukamilika
kutokana pia na Mkandarasi kudai fedha na ucheleweshwaji wa fedha zilizosalia kiasi
cha Sh. Milioni 528 za ukamilishaji wake unaotokana uwasilishwaji hafifu wa
fedha kwenda Hazina ndogo.
“Usanifu wa mradi wa jengo hili ulifanywa na Wakala
wa Majengo wa Tanzania (TBA) na hadi kukamilika unataraji kugharimu kiasi cha
Sh. Bilioni 2,635,500, 772.00 na kazi zilizosalia ni ujenzi wa ngazi kwa matumizi
ya dharula, kuweka vipoza hewa, kuweka lifti ili kuwezesha watu wenye ulemavu
kufika ofisi za juu, mfumo na vifaa vya moto na kuwekwa njia na bustani eneo la
chini,”aliwasilisha.
Balozi Sefue alikubaliana na taarifa hiyo na kuahidi
kuleta kwa wakati fedha iliyosalia ili kukamilisha ujenzi wa jengo hilo huku pia
akiwaagiza uongozi wa Mkoa kuingiza kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016
mpango wa kulikarabati jengo linalotumika sasa ambalo linaonyesha kuchaka ili
nalo liweze kutumika na idara zingine zitakazosalia baada ya kuhamia jengo
jipya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.