ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 12, 2014

TEMEKE YAANZA AIRTEL RISING STARS KWA KISHINDO.

Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Omary Rajabu (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya Philipo Edson katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa Karume.
Mshambuliaji wa wa timu ya vijana ya Temeke, Siaba Salehe (jezi nyekundu) akiwania mpira na kipa  wa timu ya vijana ya Mbeya, Kelvin Dismas (kulia) na beki Yusufu Hongoli katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Haruna Ally  (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya,Yusufu Hogoli  katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Haruna Ally (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya, Yusufu Hogoli  katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Haruna Ally (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya, Yusufu Hogoli katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.
Mshambuliaji wa wa timu ya vijana ya Temeke, Siaba Salehe (jezi nyekundu) akiwania mpira  na beki wa timu ya vijana ya Mbeya,Yusufu Hongoli (jezi namba 6) katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa huku mwenzake Elia Salengo (jezi namba 13) akijiandaa kumsaidia.

Temeke yaanza Airtel Rising Stars kwa kishindo.

Timu ya wavulana ya Temeke jana imeyaanza vyema mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwa kuifunga Mbeya 2-1 katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja wa kumbu kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Baada ya kosa kosa za hapo na pale kutoka pande zote mbili, Temeke walifanikiwa kuandika bao lao la kwanza katika dakika ya 27 kupitika kwa mshambuliaji machachali Siaba Selehe. Bao hilo lilipokelewa kwa nderemo na vifijo na mashabiki wa Temeke.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila upande ukitafuta goli na Mbeya waliweza kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Mantony Malewa aliyefanya kazi ya ziada kupangua ngome ya Temeke na kuweka mpira kimiani.

Goli hilo liliongeza kasi ya mchezo huku Temeke wakisaka goli la kuongoza kwa udi na uvumba na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 70 kupitia kwa Said Mussa.
Katika mechi ya wasichana ya fungua dimba ya wasichana, timu ya Ilala ilifanya mauji ya kuungamiza baada ya kuifunga Mwanza 6-0. Dalili za kupoteza mchezo huo kwa vijana wa Mwanza ilianza kuonekana mapema ambapo Ilala walipata goli la kwanza katika dakika ya sita kupitia kwa Rehema Abdul ambaye alifunga manne peke yake.

Abdul alifunga magoli mengine katika dakika za 38, 47 na 67 huko magoli megine yakigungwa na Arasa Abdul katika dakika za 56 na 65. Kwa ujumla Ilala walitawala mchezo katika kila idara.

Mechi nyingine zilizotarajiwa kuchezwa jana ni kati ya Zanzibar na Temeke (wasichana) na Ilala dhidi ya Mwanza (Wavulana). Mashindano hayo ya kubaina na kuendeleza vipaji ngazi ya Taifa yalitarajiwa kufunguliwa rasmi na Mjumbe wa Heshima wa shirikisho la soka la Afrika (CAF) Said El Maamry.

Wachezaji 32 watachaguliwa katika mashindano haya ili kuunda timu za wasichana na wavulana ili kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars itakayofanyika nchini Gabon baadaye mwezi huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.