ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 28, 2014

KADA WA CHADEMA AHAMIA CCM NI MWENYEKITI WA MACHINGA MWANZA.

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwiguru Mchemba akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika katika uwanja wa Furahisha katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho mwishoni mwa wiki.

NA PETER FABIAN, MWANZA.
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo chazidi kukimbiwa na Makada wake ambapo juzi Kada wake maarufu aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Pamba kukihama Chama hicho na kujiunga na CCM juzi jijini Mwanza.

Uamuzi huo wa Kada wa CHADEMA, Joseph Samwel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Machinga wa Jiji la Mwanza alieleza uwamuzi huo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mwiguru Mchemba alisema kwamba ameamua kwa ihali yake kutokana na mwenendo wa CHADEMA kuendeshwa kwa ubabe bila kufuata taratibi na kanuni za Katiba ya Chama hicho.
Joseph Samwel (mwenye kofia katikati)
“Naomba mnielewe nimeondoka CHADEMA kwa utashi wangu na sijashauriwa na kulazimishwa na mtu yeyote kwa kuwa naona Chama hicho hakina viongozi wanaoweza kutuvusha katika mto wenye mamba wengi, lakini kufukuzana bila kuzingatia taratibu na kanuni za Katiba hali iliyonikatisha tamaa na kuamua kujiengua,”alisisitiza.

Baada ya kukabidhi wa Kadi ya CCM na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwiguru Mchemba  uwanjani hapo, Samuel aliwapungia mkono na kuwambia wana Chadema waliokuwa wakisikiliza sera za CCM na utekelezaji wa Ilani ya chama hicho “Nimeamua kuitumia haki yangu ya kimsingi na kikatiba kuchukua maamzi kwa hiari yangu binafsi.” alisema 

Kada huyo alitoa sababu zilizomfanya aachane na Chadema na kujiunga na CCM ni kwanza pamoja na hali halisi iliyopo ndani ya Chama cha upinzani ambapo imekuwa ya kutimuana na viongozi wa Kitaifa kushindwa kuheshimu kanuni za Katiba iliyosajiliwa kuendesha chama hicho.

“Lakini pia sababu ya pili ni kuipenda Amani ya nchi hii inayodumishwa na Chama Cha Mapinduzi, sabau ya tatu Nimejitambua pia Chama makini ni CCM, sababu ya nne nimechoshwa na siasa za uchochezi, CCM ndicho kinachoweza kutuvusha katika mto ziwa na bahari vyenye mamba wengi kutokana na kuwa na viongozi wake wenye uwezo na sifa za kuongoza Taifa hili.” Alisema na kushangiliwa na umati wa wana CCM.

Mwanachama huyo mpya wa CCM  aliamsha shangwe kubwa zaidi alipoaga Chadema kwa kuanza kusema “CCM oyee, Kidumu Chama Cha Mapinduzi, kuanzia leo mimi ni mwana CCM Chadema kwa herini bay bay hamtanisikia kurudi huko tena nilikuwa nimepotea njia .”alisisitiza.


Akimpokea Samweli Mchemba aliwataka vijana wengine kujitambua na kubaki njia Kuu ambayo ni CCM na kuachana na Michepuko ambavyo ni Vyama vya Upinzani huku akiwatahadharisha vijana kuepuka kutumiwa na kudi na baadhi ya wanasiasa kwa manufaa yao binafisi pia wakiwatumia kufanya vurugu na uchochezi kwa lengo la kuisambaratisha Amani na Umoja wa kitaifa ulioachwa na waasisi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.