Bwa. Singili alisema kuwa Benki ya Azania ni kama
sehemu ya jamii, watajitahidi kutoa msaada kwa jamii katika Nyanja za
elimu,afya na kusaidia yatima kila nafasi na uwezo unaporuhusu.Benki ya Azania
pia iliwaalika Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo
House Foundation.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa benki ya Azania imekuwa sasa na kufikia matawi 15 ikilinganishwa na matawi matatu waliyokuwa nayo mwaka 2007,alisema kwa Dar es salaam pekee wana jumla ya matawi 05. ''tunawashukuru wateja wetu,kwani bila uwepo wao tuingefika hapa,tunapenda kuwahakikishia kuwa tunaendelea na juhudi zetu za nia ya kutaka kuwa na teknolojia ilio sahihi'',alisema MKurugenzi huyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.