WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Sera na Uratibu Steven Wasira (Mbunge wa Jimbo la Bunda) wilayani humo mkoani Mara ameongoza marafiki, wazaliwa na wafanyabiasha mbalimbali kuchangia kiasi cha Sh. 60 kati 172 katika harambe ya maendeleo ya Kata ya Nyamuswa. iliyofanyikia jijini Mwanza.
Harambe hiyo iliyoratibiwa na Mfuko wa Wazee wa Maendeleo wa Kata ya Nyamuswa iliyopo Wilaya ya Bunda ili kuhamasisha wananchi wazaliwa na walioko nje kutoka katani humo ili kuiletea maendeleo badala ya kusubiria Serikali kufanya kila jambo la maendeleo.
Awali katika hafla hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Kata hiyo Mwenyekiti wa muda Juma Makongoro aliyeratibu shughuli hiyo jijini Mwanza hivi karibuni alisema kwamba, lengo kubwa ni kukabiliana na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinayoikabiri kata hiyo.
Makangoro alieleza kuwa, harambe hiyo imelenga kukusanya kiasi cha Sh. Milioni 172 ambazo zitatumika katika ununuzi wa mashine ya kusukuma maji iliyoharibika kwenye eneo la chanzo cha maji safi katani humo, gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Nyamuswa, kujengea chumba cha kuhifadhia maiti, chumba cha kujifungulia kwa wajawazito.
Aidha aliongeza kuwa fedha hizo zitakazopatikana zitatumika pia katika kuwekea umeme kwenye nyumba za walimu na maofisi ya shule za msingi za Nyamuswa A na B, Ikizu A na B, Bukama, Busore na Sekondari ya Makongoro ili kumaliza chanmgamoto hizo zinayoikabili Kata hiyo na kusababisha kuwa kero kwa wananchi.
“Turibuni utaratibu huu baada ya kuanzisha mfuko wa wazee wa maendeleo wa Kata ya Nyamuswa mwaka 2012 kutokana na changamoto kubwa zinayoikabiri Kata yetu na ili kuzitafutia ufumbuzi ambapo tulianza na mkakati wa kuchangia kupunguza uhaba wa madawati ili wanafunzi waache kukaa chini,” alisema.
Akichangia kwenye harambee hiyo Waziri Wasira alisema kwamba, utaratibu huo umelenga kuisaidia serikali katika juhudi zake za kuwafikishia maendeleo katika Sekta mbalimbali badala ya kusubiria kila jambo kufanywa na serikali pekee jambo ambalo limekuwa likichelewesha kupatikana huduma kwa wakati na kupelekea wananchi kuilalamikia serikali na viongozi wake.
“Niwapongeze sana walioanzisha jambo hili kwa kuwa limelenga kushirikiana na serikali yenu iliyopo madarakani kutatua kero mbalimbali zilioko kwenye maeneo yetu hasa za huduma za kijamii hili lisiishie hapa tu bali liwe ni endelevu,” alisisitiza.
Katika halfa hiyo Waziri Wasira alichangia kiasi cha Sh. Milioni 5, Daniel Lameck ambaye ni Mkurugenzi wa La-Kairo Investment Co. Ltd. akichangia Sh. Milioni 2 na uongozi wa WDC Kata hiyo ukiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Max Madola ukichangia pamoja na marafiki, wafanyabiashara na wazaliwa wa Kata hiyo huku Jaji Warioba akiahidi kuchangia (kiasi hakikutajwa).
Hadi mwisho wa harambe hiyo ya kuchangia ikimalizika na mgeni rasmi DC Masenza kutangaza fedha iliyopatikana kiasi cha Sh. Milioni 60 ikwa ni tasilimu, ahadi ikiwa Sh. Milioni 40 huku mwenyekiti Makongoro akitoa wito kwa walioahidi kukamilisha ahadi zao na ambao hawakufika kuguswa na kuwasilisha michango yao na zoezi hilo kuelezwa kuwa endelevu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.