ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 27, 2014

KUONDOA SHILINGI NI MCHEZO WA KUIGIZA!


@Mwanamabadiliko
KATIKA hili bunge la bajeti linaloendelea sasa hivi, pamoja na kwamba limekosa mvuto kutoka kwa jamii ya watanzania, kuna mambo matatu nimeyagundua. Kwanza, huu utaratibu wa kuondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kama mchezo wa kuigiza kwa kuwa wabunge wanaoshika hizo shilingi hatimaye huziachia na vifungu vya ovyo vya bajeti hupitishwa.
 
Pili, kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge hili nimeshuhudia wabunge wa CCM wakiondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri wa chama chao. Nadhani ni muendelezo ule ule wa kuleta mzaha na kuwakoga wananchi wanaowatazama ili waone kwamba wana uchungu na maendeleo yao wakati si kweli. 

Lakini pia wanafanya hivyo ili kufuata mkumbo wa wabunge wa UKAWA ambao tangu mwanzo walitahadharisha kushika shilingi za mishahara ya mawaziri ambao wameshindwa kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Kinachowaponza wabunge wa UKAWA ni uchache wao kwani hata kama wakishika shilingi, mwisho wa siku wabunge wa CCM watapiga kura za Ndiyooooooooooooooo ili kuwaokoa mawaziri wao wa CCM.
 
Tatu, nimegundua kwamba mle bungeni kuna wabunge wa CCM ambao wao kazi yao kubwa wanayoijua ni kusema NDIYOOOOOOOOOOO kwa sauti kubwa ili vifungu vya bajeti, hata vile vibovu, vipite bila kupingwa. Kundi hili huwa halichangii chochote bungeni. Wakishaingia bungeni wakasaini kwenye kitabu cha posho, hukaa mezani na kusubiri kugonga meza. 

Hili ni suala la kustaajabisha sana kwani wabunge hawa wametumwa na wananchi waende kuwawakilisha lakini wamegeuka kuwa wachumia tumbo na watetezi wa ukandamizaji wa serikali dhidi ya wananchi. 

Na kwa kuwa moja ya kazi ya wabunge ni kuibana serikali iwahudumie wananchi, wabunge hawa wa CCM ni wasaliti wa wapiga kura wao na hawafai kurejeshwa bungeni tena msimu ujao. Inasikitisha sana kuona kwamba wabunge hawa wa CCM wapo bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wananchi badala ya kuwatetea!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.