Ofisa wa maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba akiwasilisha mada katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kwa waandishi wa habari mkoa wa Mwanza. |
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari wameshiriki warsha hiyo. |
Vyombo vya habari ndiyo msingi wa kutoa elimu kwa jamii. |
Mmoja kati ya waandishi wa habari toka City Fm ya jijini Mwanza akichangia kwa kuuliza maswali. |
Ingawa Ziwa Victoria limekuwa chanzo cha kukuza uchumi wa Taifa kupitia mazao ya samaki, lakini shughuli za uvuvi haramu ndiyo sababu za kuporomoka kwa uchumi wa mkoa wa Mwanza na taifa kwa ujumla. |
Kikazi zaidi warshani. |
Wadau wa Bodi ya maji Bonde la Ziwa Victoria waliketi hapa kila mmoja na wakati wake aliwasilisha mada na kujibu maswali. |
Mtaalamu wa maji ya ardhii Magasa Ogoma akiwasilisha mada. |
Ofisa wa maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba akizugumza na wandishi wa habari. |
WANANCHI KANDA YA ZIWA WAHIMIZWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI.
BODI ya Bonde la Maji Ziwa Victoria (LVBWB) imewataka wadau wa mazingira na watumiaji wa maji kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji.Wito huo umetolewa na Afisa wa Maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba wakati akiwasilisha mada ya usimamizi wa rasilimali za maji kwa pamoja katika warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari jijini Mwanza.
Alisema ili utunzaji wa vyanzo vya maji na rasilimali za maji katika bonde la Ziwa Victoria, mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa ni pamoja na kuwapo kwa usimamizi wa pamoja, ushirikishwaji wa sekta ikiwa ni pamoja na usitishaji wa shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.
Alisema ushirikiano wenye tija unahitajika na kutaja sekta za Madini, misitu, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda na Utalii kama maeneo yanayopaswa kushirikiana katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji.
"Ili kulinda Bonde la Ziwa Victoria, ni lazima kuwepo na sera ya pamoja kwa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zinazowiana katika utunzaji wa rasilimali za maji katika maeneo ya nchi hizi, pia utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kwa wadau na wananchi ili kuwezesha jamii inayozunguka vyanzo vya maji kutambua faida na umuhimu wake" alisema.
Mpemba ameshauri kuwako kwa mpango utakaositisha shughuli zote za kibinadamu zinazofanywa karibu na vyanzo vya maji kama Mahoteli na Viwanda kuzuia uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji, na katika sekta ya uvuvi kuzingatia kanuni za uvuvi endelevu ili kujihakikishia ukuaji wa kiuchumi unaotokana na zao la samki ziwa Victoria.
Pia Afisa huyo amewataka wananchi na makampuni yanayotaka kutumia maji ya Ziwa Victoria au kuchimba visima kuomba vibali vya kufanya utafiri wa maji ardhini kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kwani ndivyo inavyosema katika kunusuru ziwa hilo na vyanzo vyake kwa matumizi yasiyofaa.
“Maji ni rasilimali ya kiuchumi,ni vyema ikafahamika kuwa wananchi hawana budi kuchangia gharama kidogo ili rasilimali hii iendelee kuwepo na sheria ya rasilimali za maji ya mwaka 2009 kifungu cha 96 na 112 inamtaka kila mtumiaji maji apate kibali cha kutumia maji kwa kuomba katika ofisi ya maji,Bodi ya Bonde husika.
“Lakini wapo wananchi wachache wenye uelewa kuhusu sheria hii wamejitokeza na kuomba vibali na kulipia ada ya matumizi ya maji ,hivyo ni vyema kila mtumiaji wa maji akaitekeleza sheria hii ili kuepuka adhabu ya kuivunja.
“Sheria ya rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 kifungu cha 102 kifungu kidogo cha 2 inatamka yeyote atakaye kaidi kuitekeleza adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi laki tano au isizidi shilingi milioni moja na kama ataendelea kutolipa atatozwa faini ya shilingi milioni moja au kwenda jela miaka si chini ya mitatu”alisema
Aliongeza kuwa ili kufikia malengo ya pamoja shughuli zote za usimamizi wa matumizi ya maji ya rasilimali hiyo zinapaswa kujiendesha zenyewe, hivyo kulipa ada ya matumizi ya maji kwa wakati ni kuchangia katika uboreshaji huduma ya maji itakayo saidia kusimamia matumizi bora ya rasilimali hii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.