ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 26, 2014

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA KISASA LA HUDUMA KWA WATEJA MWANZA.

Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Christopher Fuime akisalimiana na wafanyakazi wa Airtel tawi la Mwanza kabla ya uzinduzi wa duka la huduma za mtandao zinazotolewa na kampuni hiyo lililopo katika makutano ya barabara ya Kenyata na Stesheni Nyamagana jijini Mwanza al maarufu 'Kipleti cha Samaki'. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Airtel Adriana Lyamba.  


Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Christopher Fuime ambaye alimwakilisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi Valentino Mlowola akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka la huduma za Airtel tawi la Mwanza huku akishuhudiwa kwa karibu na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Airtel Adriana Lyamba pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.


Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Christopher Fuime alitembezwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Airtel Adriana Lyamba ndani ya jengo la duka hilo kujionea maboresho yaliyofanyika ikiwa ni sambamba na shughuli zinavyofanywa na vitengo mbalimbali. 
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Christopher Fuime akipata maelekezo juu ya utoaji wa huduma ulivyoboreshwa ili kuendana na kasi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa wateja kwa kujali muda na wakati.
Kamanda Fuime amesema kuwa ili kukabiliana na wezi, walaghai na wahujumu wa fedha za mitandao ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi ndiyo utaweza kuwatia nguvuni wabaya hao. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.

"Hilki ni kitengo cha mauzo ya simu za mkononi kuanzia bei za chini nafuu kwa mteja hadi simu za viwango vya juu zenye uwezo wa kutandaza na kupokea huduma mbalimbali, tumekiweka hapa kuwarahisishia wateja wetu mpango wa kupata simu zilizo bora kwa bei "  alisikika Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba (kulia) akitoa ufafanuzi mara baada ya kuzinduliwa kwa duka la Huduma kwa wateja la kwa kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa Airtel jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba amesema kuzinduliwa kwa duka hilo jijini Mwanza kutaongeza kasi ya utoaji wa huduma kwa wateja zinazolingana na mahitaji ya wateja wa kampuni hiyo.


Amesema kuwa huduma bora na za haraka ni dhamira ya Airtel kuhakikisha wateja wa Tanzania na Africa kwa ujumla wanapata huduma bora na salama. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.

Afisa mauzo wa Airtel Kanda ya Ziwa Violet Gyumi akitoa zawazi kwa wateja waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa duka la Airtel Mwanza.
Afisa mauzo wa Airtel Kanda ya Ziwa Violet Gyumi (katikati) akiwa na moja ya maafisa wa Airtel (kulia) wakitoa zawazi kwa wateja waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa duka la Airtel Mwanza.
Wafanyakazi wa Airtel tawi la Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja.


"Mgeni yeyote atakaye ingia duka hili hatotoka kapa". Pichani Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Airtel Adriana Lyamba akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Christopher Fuime mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa duka la huduma za mtandao zinazotolewa na kampuni hiyo lililopo katika makutano ya barabara ya Kenyata na Stesheni Nyamagana jijini Mwanza.
Picha ya pamoja: Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Christopher Fuime, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Airtel Adriana Lyamba pamoja na wafanyakazi wa Airtel tawi la Mwanza baada ya uzinduzi wa duka la huduma za mtandao zinazotolewa na kampuni hiyo lililopo katika makutano ya barabara ya Kenyata na Stesheni Nyamagana jijini Mwanza.
Airtel yafungua duka la kisasa Mwanza
Mrakibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime,  ameipongeza Airtel kwa kuboresha mazingira ya maduka yao  kuwa ya kisalama zaidi kwa watumiaji wa huduma zao mbalimbali husasani ya Airtel Money.

SSP Christopher Cyprian Fuime,   aliyasema hayo kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola  wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa la Airtel lilipo Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki hii.

SSP Fuime alisema” nimefurahishwa sana na maboresho makubwa katika duka hili  ambayo yatawawezesha wakazi wa Mwanza na wateja wa Airtel kupata huduma bora kwa haraka zaidi katika mazingira mazuri. Duka hili sasa linawahakikishia watej usalama zaidi  wanapofanya miamala ya fedha kupitia counter maalumu zilizowekwa kwaajili ya kuhakikisha usalama wa wateja na mali zao. Sisi kama polisi tulionadhamana ya kuhakikisha usalama wa raia tunawapongeza sana Airtel kwa kuliona hili na kuhakikisha huduma ya Airtel Money inatolewa katika mazingira yaliyo na usalama”.
“Tunawashauri wateja na wakazi wa Mwanza kupata muda na kutembelea duka hili na kufurahia huduma zinazotelewa hapa”. Aliongeza SSP Fuima

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alisema” Tunaendelea na mradi wetu wa kuboresha maduka yetu na kuyafanya yawe ya kisasa zaidi , leo tunazindua duka letu la mwanza baada ya matengenezo, mwonekano huu mpya ulioboreshwa zaidi utatuwezesha kutoa huduma kwa ufanisi , haraka zaidi kupitia kaunta zilizowekwa kwaajili ya kuhudumia wateja. sasa wateja watahudumia kwa haraka bila kupoteza muda.

Sambamba na hilo tumeboresha sehemu za kutoa na kutuma pesa kwa kuweka kaunta maalumu zilizo za kisalama zaidi zitakazowawezesha wateja wetu kutumia huduma ya Airtel Money kwa usalama zaidi.

Huu ni mwanzo tu katika kuhakikiksha tunato huduma bora na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu. Mpango ni kufungua matawi zaidi na kuboresha maduka yetu yote nchi ili yawe ya kisasa kama hili la mwanza, Arusha na Mlimani City Dar ambayo tayari tumeshayazindua aliongeza Lyamba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.