MVUTANO kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi wilayani Geita kuhusiana na ujenzi wa choo katika soko lililoko mjini Geita hatma yake itakwenda kujukana kesho mara baada ya kikao cha leo (Jumatatu) kufanyika kikiitishwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw Saidi Magalula ambapo amenuia kukutana na wadau wa soko hilo.
Mgogoro huo ambao unafukuta na kudaiwa kusababisha mvurugano wa sintofahamu unadaiwa kuleta mvutano mkali ndani ya chama hicho ambapo Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Mji wa Geita, Bw Martin Kwilasa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Bw Joseph Msukuma wanalumbana kuhusiana na ujenzi wa choo ambao unaendelea kujengwa katikakati ya soko la mji wa Geita lenye thamani ya shilingi milioni tisini (90,000,000/=)
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bw Joseph Musukuma wakati akiongea mwishoni mwa wiki na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya La Cairo Mei, alidai kuwa hatoendelea kuruhusu ujenzi wa choo hicho uendelee katikati ya soko hilo na badala yake choo hicho kijengwe nje ya soko kulingana na ramani ya awali.
Alitoa sababu ya ujenzi huo kufanyika ndani ya choo hicho ni kutokana na eneo ambalo awali lilitengwa kujengwa choo hicho kugawiwa Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Mji wa Geita na zoezi hilo lilibalikiwa na asilimia kubwa ya madiwani katika baraza hilo ambalo alidai kuwa hata hivyo baadhi yao hawajui kusoma na kuandika na ambao wana elimu ni ya kuungaunga kama ilivyo bunduki…mbele chuma nyuma ubao.
Alidai kuwa baadhi ya madiwani katika halmashauri hiyo wamekuwa wakirubuniwa na baadhi ya maofisa katika halmashauri hiyo na kusaini mikataba ambayo haiendani na matakwa ya wananchi kutokana na baadhi yao kuwa na elimu ndogo na kutoa mfano wa Mameya wa Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Jiji la Mwanza waliodaiwa kukubwa na matatizo ya kusaini mikataba mibovu iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza.
Alisisitiza kuwa choo hicho hakiwezi kujengwa kutokana na kutetea kauli ya wananchi ambao wanafanya biashara katika soko hilo ambao walipeleka malalamiko yao na kuyafanyia kazi kwa kuyaona kuwa ni ya msingi na kusitiza ujenzi huo kwa kusaidiwa na jeshi la polisi na kuongeza kuwa kauli yake ni ya mwisho kwa kufuata sera zinazoongoza chama cha CCM.MSIKILIZE MWENYEKITI WA CCM MKOA WA GEITA AKISIMULIA MKASA MZIMA.
Akijibu tuhuma hizo, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Mji wa Geita, Bw Martin Kwilasa alisema kuwa maamuzi ya ujenzi wa choo hicho katikati ya soko yalitolewa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi Aprili 28, mwaka huu ambapo kikao kilibariki mapendekezo hayo kuwa choo kijengwe katikati ya soko.
Alisema kuwa anashangaa kuona maamuzi ya mwenyekiti huyo yakitokea yakipinga ujenzi wa choo hicho kisijengwe na kusema kuwa Mei, 16 mwaka huu mwenyekiti huyo aliongoza wananchi kwenda kufukia shimo la choo hilo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi jambo ambalo alisema kuwa ni kigeugeu na hatakiwi kuongoza wananchi kutokana na kutokuwa na msimamo.
Alisema kuwa ujenzi wa choo hicho katikati ya soko ni kutokana na mkataba kati ya wafadhiri ambao ni COWI Tanzania Ltd kutoka jijini Dar es Salaam ambao wanafadhili mradi huo kwa gharama ya shillingi milioni 90,000,000 ambao wamejenga vyoo kama hivyo katika nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
Aidha kuhusiana na elimu ya madiwani katika baraza hilo, alisema kuwa wao wana elimu ya kutosha na wanakubalika kwa wananchi na wako makini zaidi hakuweza kufafanua zaidi.
Saidi Maneno Kalidushi ambaye ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Geita amelaumu kitendo cha kiongozi huyo kutengua agizo la Mwenyekiti wa Mkoa kwani siyo utaratibu na kusema kuwa suala hilo litafikishwa kwenye kamati ya maadili. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.
Waandishi wa habari. |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bw Joseph Musukuma ameongeza kwa kusema kuwa shughuli nyingi za serikali hapa nchini hukwamishwa na watendaji wachache ambao hupewa dhamana ya kuwa wataalamu wa Halmashauri mbalimbali kwa kutoa maamuzi yaliyo egemea maslahi binafsi ambayo mwisho wa siku huigharimu serikali kwa kuipa hasara. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.