Kigwangala Atafakari
Urais 2015
Mbunge wa jimbo la Nzega
Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala, ametanabaisha kuwa anatafakari
kama anaweza kugombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha
mapinduzi CCM.
Akijibu maswali ya
waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye baadhi ya
mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa mara
inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema anatafakari
jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika atayazingatia maoni ya
wananchi.
Akizungumzia maelezo
kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba anataka kuwa
kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk. Kigwangala alisema
yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala hajamtuma mtu kuanza kumfanyia
kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na katiba yenye Uhuru wa kujieleza na
kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao na wana haki ya kufanya hivyo na yeye
binafsi hawezi kuwapinga.
Hivi karibuni kumeibuka
mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wanaharakati
kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala kuchukua fomu ya kugombea
Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ifikapo mwaka 2015.
Mijadala hiyo mizito
imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi walio ipachika jina
"Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala hiyo wamekuwa
wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba ndiye kiongozi pekee
anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya vijana
wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta upinzani wa kweli
kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na misimamo na uwezo wa
kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.
Dk Kigwangala ni mbunge
wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya udaktari wa tiba ambaye pia
ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za
mitaa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.