Airtel Tanzania. |
· Wateja sasa kufurahia huduma bora katika muonekano mpya na wakisasa
· Sasa wateja kufaidika na bidhaa na huduma nyingi zaidi dukani hapo
Airtel Tanzania mwishoni mwa wiki hii imezindua duka la Mlimani City baada ya kulifanyiwa matengenezo na kulipatia sura ya kisasa zaidi. Uzinduzi huu ni kielelezo cha kampuni hiyo kutoa huduma bora za simu kwa wateja wake.
Akiongea wakati wa uzinduzi Christophe Soulet, Afisa Mtendaji Mkuu Africa alisema” Airtel tunaamini katika kutoa huduma bora za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu huku tukiwapa uzoefu wa pekee katika huduma zetu. Mpango huu wa kuboresha maduka yetu unafanyika katika masoko yetu yote yaliyoko barani Afrika na Leo ninayofuraha kuzindua duka hili la kisasa lijulikanalo kama Express shop hapa nchini Tanzania. Duka hili la kisasa linathibitisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” duka hilo ni la kwanza kuzinduliwa kwani tunabadilisha maduka yetu yote nchi nzima na kuyafanya yawe na mtazamo mpya na wa kisasa zaidi. Duka hili limetengenezwa na kuhakikisha mteja ataweza kupata huduma kwa haraka , kwa usalama bila usumbufu wowote.
Aliongeza kwa kusema Airtel inapenda kuwahakikishia wateja kupata huduma bora wakati wote na pia kupata simu za aina mbalimbali ambazo zitapatikana katika duka hilo jipya la Mlimani City.
Kwa kupitia mtandao wetu mpana ulionea zaidi tunawahakikishia wateja wetu huduma bora za kisasa, za uhakika jijini Dar es salaam.
Duka la Mlimani City litaendelea kuuza bidhaa mbalimbali kama vile modem na simu za aina mbalimbali , wateja watapata huduma ya Airtel money kwa usalama zaidi , kuunganisha na huduma za simu za malipo ya mwenzi na ya awali , pamoja na huduma za internet na kuunganishwa na mtandao na kuperuzi kwenye internet , kununua muda wa maongezi pamoja na huduma nyingine nyingi.
Airtel Tanzania inaendele kuboresha huduma zake kwa wateja ambapo inaendele kuboresha maduka yake nchini nzima kwa mwaka huu wa 2014. Mpango ni kuwafikiwa wateja wengi zaidi na kuboresha huduma zake kupitia maduka yake yote yaliyoko nchi nzima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.