RUCCO Iringa mabingwa wa Taifa Safari Pool 2014.
Na Mwandishi
Wetu.Moshi
CHUO cha RUCCO
cha mkoani Iringa kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool Taifa
yaliyoyoshirikisha mabingwa wa Vyuo vya Elimu ya juu kutoka mkoa minane yajulikanayo
kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014” mwishoni mwa wiki katika Ukumbi
wa Aventure Moshi -Kilimanjaro.
RUCCO
ilifanikiwa kupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha St. John cha Dodoma 13-12,
na hivyo kuzawadiwa kikombe na fedha taslimu
Shilingi 2,500,000/=
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na St. John ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi
1,500,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na chuo cha Ardhi cha Dar es Salaam kwa
kukifunga chuo cha Muccobs 13-8 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
1,300,000/= na nafasi ya nne ikaenda kwa wenyeji wa mashindano hayo Muccobs
ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,000,000/=
Timu zingine
ambazo hazikufanikiwa kufikia hatua ya nne bora zilizawadiwa kifuta jasho cha
fedha taslimu shilingi 500,000/= kwa kila chuo ambavyo ni chuo cha
TIA,Bugando,Sua na Mzumbe.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja Wanaume,Fredrich Mwangata kutoka chuo cha SAUT Mwanza
alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Taifa na kuzawadiwa Ngao pamoja na fedha
taslimu Shilingi 300,000/=
kwa kumfunga Steven Kyasi kutoka Chuo cha Mzumbe Mbeya 4-0,ambaye
alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=
Nafasi ya
tatu ilichukuliwa Justus Mhando kutoka chuo cha Mipango Dodoma ambaye alizawadiwa
Shilingi 150,000/= na nafasi ya nne alichukua Ally Jamson wa Muccobs Moshi na kuzawadiwa
100,000/=.
Upande wa
kinadada Jacline Molel kutoka chuo cha TIA alitwaa ubingwa wa Taifa na
kuzawadiwa ngao pamoja na fedha taslimu Shilingi 200,000/= kwa kumfunga Deborah
Ramadhani kutoka chuo cha SILA Arusha
3-0 na hivyo Debora kushika nafasi ya pili na kuzawadiwa Shilingi 150,000/=.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Rehema Uzi kutoka Chuo cha UDOM ambaye
alizawadiwa Shilingi 100,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na Beatrice Madafu
kutoka RUCCO ambaye alizawadiwa Shilingi 50,000/=
Fainali za
Kitaifa zilishilikisha mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma,
Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014,Mkoa
wa Kilimanjaro.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.