ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 5, 2014

JERNIFER YESE AJISHINDIA LUNINGA SHINDANO LA KUNYWA KUSANYA NA USHINDE NA COCA COLA.

NA ALBERT G. SENGO; MWANZA
Hatimaye mshindi wa kwanza wa Luninga kupitia shindano la Kunywa Kusanya na Ushinde linaloendeshwa na kampuni ya vinywaji baridi nchini Coca Cola amepatikana hii leo jijini Mwanza.

Akimtangaza mshindi huyo Meneja wa mauzo wa Nyanza Bottling Company limited ya jijini hapa Marko Masaka, amemtaja Bi. Jernifer Jesse kuwa ndiye mshindi pia akatoa wito kwa wanywaji wa soda kutopuuzia kuchungulia chini ya vizibo mara tu wanapo nunua bidhaa hizo na kuzinywa kwani watapoteza bahati ya kujishindia zawadi kemkem zikiwemo za Luninga zitakazo wapa fursa kuona michuano ya soka Kombe la dunia kwa ubora, sambamba na kujishindia zawadi nyingine kama Tiketi ya michuano hiyo mikubwa ya soka, T-shirts na Mipira. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Meneja wa mauzo wa Nyanza Bottling Company limited ya jijini hapa Marko Masaka (L), akimkabidhi mshindi wa Luninga Bi. Jernifer Jesse aliyeshinda kupitia shindano la Kunywa, Kusanya na Ushinde linalo endeshwa na kampuni ya vinywaji baridi nchini Coca Cola.
Mshindi wa Luninga Bi. Jernifer Jesse (L) aliyeshinda kupitia shindano la Kunywa, Kusanya na Ushinde linalo endeshwa na kampuni ya vinywaji baridi nchini Coca Cola akisaidiwa na rafikiye kubeba zawadi alojishindia hii leo.
Ni zawadi kemkem zikiwemo za Luninga zitakazo wapa fursa kuona michuano ya soka Kombe la dunia kwa ubora, sambamba na kujishindia zawadi kubwa ya Tiketi ya kwenda kushuhudia michuano ya kombe la dunia. 
Vipi kuhusu T-shirts na Mipira?
Mshindi wa Luninga ya kwanza Bi. Jernifer Jesse aliyeshinda kupitia shindano la Kunywa, Kusanya na Ushinde linalo endeshwa na kampuni ya vinywaji baridi nchini Coca Cola akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Nyanza Botling Co. LTD vilivyoko Igoma jijini Mwanza. Shindano bado linaendelea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.