Na Peter Fabian
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA.
MCHEZAJI Chipukizi wa timu ya Alliance cademy Athanas Mudaula (17) aliyeteuliwa kwa mara ya kwanza na kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars amevisa vilabu vikubwa nchini na mataifa ya nje kumpatia nafasi ya kuzingatia masomo kwanza kwa muda badala ya kumkodolea macho na kukimbilia kumsajili kuvitumikia.
Mudaula amesema hayo juzi wakati alipoalikwa kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga aliyeutaka uongozi wa shule ya Sekondari Alliance na Kituo cha Academy anachotoka kijana huyo kumpeleka ofisini kwake kumtambulisha rasmi na kupata fursa ya kuzungumza naye na kumpa busara zake za kumjenga mchezaji huyo chipukizi aliyepata kurejea kutoka Jijini Namibia na Dar es salaam kutekeleza majukumu ya kuitumikia timu ya Taifa (Taifa Stars).
Chipukizi
huyo amesema kwamba tangu kuteuliwa kwake kujiunga na kuchezea taifa stars
ameanza kupata usumbufu kutoka viongozi wa vilabu vikubwa kuanza kuwasiliana na
uongozi wa Kituo Alliance wakiomba hata kumhamisha shule akasome ambako vilabu hivyo vinadhani itakuwa rahisi kumtumia.
“Mimi
bado ni mwanafunzi nahitaji kwanza kusoma na kukiendeleza kipaji change kwani
hata ushauri niliopewa na Mkuu wa Wilaya Konisaga baada ya kukutana naye leo
ameniasa zaidi kusoma na ushauri wake huo imeonyesha kunilenga mimi na kutaka
niweke bidii kwenye masomo ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu na maadili ya
soka ili kuwa mchezaji wa kiwango cha kimataifa name ntauzingatia” alisema. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)
Mudaula
ambaye ni mchezaji wa timu ya Alliance chini ya umri wa miaka 17 (U-17) ambaye
aliweza kuingia kipindi cha pili katika mchezo kati ya Taifa stars na Namibia
ambapo matokeo ya mchezo huo yalikuwa sare ya bao 1-1 na kuwekwa historia ya
kituo hicho kumtoa chipukizi kuchezea timu ya taifa na kufuata nyayo za shule
ya sekondari Makongo.
“Dhamira
yangu mimi kwanza ni kusoma ili niweze kufikia malengo na kuwa mchezaji wa
kimataifa kama tunaowasikia na kuwaona kwenye runinga hivyo nitaendelea
kuzingatia maadili.
Naye
Mkuu wa Wilaya Konisaga amempongeza mchezaji huyo pamoja na kuwa na umri mdogo
lakini kipaji chake na kujituma kwa kufuata vyema maelekezo ya walimu ndiyo
kimewapa nafasi Makocha na Viongozi wa TFF kumteuwa na kumjumuisha kuwemo
kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Namibia na kuitangaza Alliance na Wilaya ya Nyamagana
kitaifa na kimataifa.
“Zingatia
masomo kwanza ili kufikia malengo pamoja na kipaji chako pia unao vijana
wenzako sasa wewe ni balozi wao utakayewawakilisha na wachezaji wote nyota wana
akili za kuzaliwa na hata za darasani sasa zingatia elimu kwanza huku pia
ukiendeleza kukilinda kipaji chako kwa nguvu zote”alisisitiza.
Konisaga
aliwataka wazazi na walezi wa vijana wote walioko kwenye shule za msingi,
sekondari na vyuo mbalimbali vikiwemo vikuu kuhakikisha wanawalea vyema vijana
wenye vipaji na kuacha dhana kwamba vijana wataegemea kwenye michezo na kuacha
masomo ya kitaaluma jambo sio la kweli kwani shule za Alliance kitaaluma
zimefanya vizuri kufaulisha wanafunzi kwa daraja la kwanza nala pili na
kuwezesha kuongoza kiwilaya hadi kitaifa.
"Wito
wangu kwa wananchi, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali, mashirika na kampuni wakiwemo
wadau wa maendeleo kujitokeza kusaidia sekta ya michezo katika timu mbalimbali
zilizopo Wilayani Nyamagana na Jiji la Mwanza zinazoshiriki mashindano kuanzia
ngazi za mtaa hadi ligi kuu jambo ambalo litaongeza chachu ya kukuza soka na
kuwezesha kupatikana wachezaji wengi wenye vipaji vya soka "
“Mchezaji
star yoyote duniani ni lazima awe na akili kwanza anatumia akili anapokuwa
uwanjani hivyo ni vyema sasa mkatambua kuwa vijana ni lazima wapate elimu ili
kumuwezesha kuwa mchezaji wa kimataifa ambaye atakuwa mtambuzi wa lugha za
kimataifa na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufasaa zaidi wakati
wakupata maelekezo kutoka kwa makocha na hata wachezaji wenzake uwanjani”
alisema Konisaga.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shule za Alliance na Kituo cha Alliance Academy James
Bwire alisema kwamba kuteuliwa kwa kijana huyo kuchezea timu ya taifa stars na kwenye
timu ya taifa ya waliteuliwa vijana sita kujiunga na Airtel releasing star
walichaguliwa vijana watatu akiwemo Mudaula ambao walishiriki mashindano hayo
nchini Naigeria na kuibuka mfungaji bora wa mashindano hayo hivyo anacho
kipaji.
“Sisi
Alliance ndo tunaomsomesha na kuendeleza kipaji chake kijana Mudaula lakini
alipoteuliwa tu kujiunga na kuichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza akitokea
Kituo cha Alliance Academy kwenye mchezo wa kirafiki wa kutekeleza Kalenda ya
FIFA na timu ya taifa ya Namibia na kutoka sare, sasa tumeanza kupata maombi
kutoka klabu za Azam (Tanzania), Al Ahal (Misiri), Harambee (Kenya) na baadhi
ya timu tatu za nchini Namibia” alisema.
Wito
wangu kwa wadau mbalimbali wa michezo na wafanyabiashara, taasisi, mashirika na
makampuni kujitolea kukisaidia kituo cha Alliance ambacho kwa sasa kina timu
inashiriki ligi daraja la nne Wilaya ya Nyamagana na kwenye mashindano
mbalimbali yanayoanzishwa na kituo hicho na inayoshiriki kitaifa na kimataifa
ili kuendeleza vipaji kwa vijana wa umri wa miaka 17, 15 na 7 wa Alliance
Academy.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.