Ameongeza kuwa ACT Tanzania kimekuja na dhamira ya dhati ikiwa imejengwa na mfumo wa ukweli na uwazi tangu kuanzishwa kwake na jinsi kitakavyoongozwa misingi yake na malengo yake vyote vimelenga kumkomboa mtanzania mnyonge.
"Vyama vingine vyote vinaitikadi inayojali nguvu ya soko, na sisi (ACT) tunasema mtanzania ambaye amekosa elimu asiye na mtaji huwezi kumsukuma kwenye soko huria akaenda kushindana na wafanyabiashara wenye mitaji, hivyo ACT haitaliruhusu hilo liendelee na badala yake tutaleta usawa katika jamii na kumwezesha mwananchi kujiendeleza kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo " alisema Mwigamba.
Bendera ya ACT Tanzania. |
Mweyekiti Limbu akiendeleea kutoa msisitizo kuhusu dhamira ya chama hicho kipya. Kulia ni Pendo Ojijo (mmoja kati ya wanachama wa ACT) |
Kusanyiko la Viongozi, wanachama na wanahabari katika ukumbi wa hotel ya JB Belmonte jijni Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.