Wathilika wa mafuriko wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq |
Kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd
yakabidhi magodoro kwa waathirika wa mafuriko Dakawa, Moro
Na Mwandishi
Wetu, Morogoro
Kampuni ya Pan
Africa Enterprises Ltd imetoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya
waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na
kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi.
Akikabiddhi
Jumuiya ya
Wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam wametoa vitu vyenye thamani ya shilingi
milioni 117/- katika kuwasaidia wahanga wa mafuriko katika vijiji vya Magole na
Mateteni vilivyoko wilaya Kilosa, mkoa wa Morogoro.
Akizungumza
wakati wa kumkabidhi Mkuu wa Moka wa Morogoro vitu mbali mbali vilivyotolewa
na wafanyabiashara wa Dar es Salaam,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick alisema kuwa wafanyabiashara wa
mkoa wake wameweza kutoa vitu mbali mbali kama vile nguo kwa kina mama vikiwemo
vitenge na khanga.
Vitu vingine
viliyotolewa na wafanyabiashara wa Dar ni pamoja na vyakula mbali mbali kama
vile sukari, mchele, maji ya kunywa, unga pamoja na vyombo vya kulia chakula.
“Hali hii ya
wahanga wa mafuriko imeweza kuwagusa kwa kiasi nkikubwa wafanyabiashara wa Mkoa
wa Dar es Salaam ambao kwa pamoja wameweza kusaidia vitu hivi vyenye thamani ya
shilingi milioni 117,” alisema
Wafanyabiashara
waliosaidia vitu hivyo ni pamoja na
Basic Elements kampuni tanzu ya Simon Group waliotoa tani 15 za unga wa
sembe wenye thani ya shilingi milioni 15, Home Shopping Centre waliotoa mifuko
1000 ya saluji pamoja na vifaa vya kulia chakula pamoja na Pan Africa
Enterprises Ltd Group ambao wametoa magodoro 200 aina ya comfy.
Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro Joel Bendera alishukuru msaasa huo uliotolewa na wafanyabiashara
hao na kusema kwamba wataugawa kwa ufasaha ili uweze kuwasaidia wahanga wote wa
mafuriko.
“Tunatarajia
kuugawa msaada huu wa chakula na vifaa kwa wahanga wote ili uweze kuwasaidia
kwa hali na mali, mpango tulionao ni kuwapatia chakula hata cha mwezi mzima ili
waweze kufanya shughuli zao nyingine kama vile kiliomo na biashara zao”
alisema.
Mkuu huyo wa
Mkoa alisema kuwa kamati ya maafa ipo mbioni kutoa ripoti nzima ya maafa hayo
ili kuwezesha jamii kujua athari nzima ya mafuriko hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.