ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 3, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI YALIVYO ADHIMISHWA MKOANI MWANZA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mwanza Aishieli Sumari akitoa hotuba kwenye kusanyiko la maadhimisho hayo ya sheria mkoani Mwanza.
Katika hotuba yake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mwanza Aishieli Sumari, aliainisha -:Masuala yanayokwamisha utendaji haki kwa kesi kuamuliwa kwa wakati,
-:Changamoto toka kwa vitengo vya Makarani, Walinzi na Mahakimu,
-:Washitakiwa nao wananafasi katika suala la utoaji haki kwa wakati kwani kwa kukataa kukiri makosa wanasababisha kesi nyingi kuendelea kusongamana kwenye mahakama zetu nchini.
Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali Kanda ya Mwanza Timoth Vitalisti akitoa hotuba juu ya hatua zilizo wekwa hatimaye kukabiliana na changamoto ya mrundikano wa kesi unaosababisha ucheleweshaji wa kesi Kanda ya Mwanza.
Safu ya jeshi la polisi nchini pamoja na jeshi la magereza ni moja kati ya wadau wakubwa wa usimamizi wa kesi pamoja na mwenendo wake kwa shughuli za uchunguzi, ulinzi wa ushahidi na masuala mengine ya msingi. 
Ni sehemu tu ya baadhi ya wanasheria wa Mahakama mbalimbali za jijini Mwanza waliojitokeza viwanjani hapa kushiriki Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyoadhimishwa mkoani Mwanza katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Kwa umakini.
Ni sehemu tu ya baadhi ya wanasheria wa Mahakama na wazee wa mabaraza ya wa mahakama mbalimbali za jijini Mwanza waliojitokeza viwanjani hapa kushiriki Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyoadhimishwa mkoani Mwanza katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika Gaspel Mwanariera amesema kuwa "Keshi nyingi nchini zimerundikana mahakamani kutokana na watendaji wengi wa mahakama hizo kwenda masomoni bila kuwepo mbadala wake hivyo kupelekea kesi nyingi kupewa  waliobaki ambao hushindwa kuzimudu kutokana na kuzidiwa na wingi, kutakiwa kuzipitia upya sanjari na kuwasoma mashahidi wa kesi hizo" 
Mhe. Angelo Rumisha ambaye ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama kuu mkoa wa Mwanza akitoa utaratibu kama mmoja wa wasimamizi wa utaratibu wa sherehe hizo.
Burudani ilihusishwa hapa! Wazee wa kazi vitengo mbalimbali vya sheria walipata fursa kutoana jasho.....mpango ambao ulinogesha kweli kweli sherehe hizo... Ilikuwa safi sanaAAaa!!.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.