ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 2, 2014

MRADI WA TIBU HOMA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA WAADHIMISHWA JIJINI MWANZA.

Mradi wa Tibu homa halmashauri ya jiji la Mwanza umeadhimishwa rasmi siku ya Ijumaa katika viwanja vya kituo cha mabasi Igoma wilayani Nyamagana ambapo samamba na mkutano wa utoaji elimu pia wazazi walipata fursa ya kupima afya za watoto wao wenye umri wa chini ya miaka mitano na kupewa tiba bure.
Mradi huu unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani (kupitia shirika la misaada USAD), ukilenga kupunguza vifo vya watoto wa chini wa umri wa miaka mitano, vinavyosababishwa na magonjwa yanayoambayana na homa, kwa mfano Maralia, Nimonia na Kuharisha.
Akina mama kama ada yao walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wana watoto wao wanapima afya kujua kama kuna mapungufu yanayo hitaji tiba, sanjari na hilo akina baba nao walikuwa mfano mzuri (kama anavyoonekana baba na mwanae kushoto pichani)
Ingawa vifo vya watoto chini ya miaka mitano bado ni tatizo kubwa duniani, na hasa katika nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara, Takwimu za sensa ya afya ya mwaka 2010 nchini Tanzania zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimeshuka kutoka 112 mpaka kufikia 81 kati ya watoto 1000 waliozaliwa hai.
Kundi hili la sanaa lilifanya igizo safi sana kuhusu masuala ya afya likihamasisha kuondokana na imani potofu za kuamini ushirikina.
Diwani wa kata Mahina Mhe. Fasheni amesema kuwa ana matumaini kuwa huduma kama hizi zitasaidia jamii kupata ufahamu sahihi kuhusu magonjwa yanayoambatana na homa kwa watoto chini ya miaka mitano na namna ya kuwasaidia.
Jamii imeaswa pia kuendelea na utamaduni wa kupima afya zao na watoto wao ili kujilinda.
Wadau wa mradi.
Ujumbe kwa mabango.
Ukaguzi kwa mabanda ya tiba ulifanyika.
Huduma zikiendelea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.