ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 8, 2013

HAPA NA PALE WILAYANI TARIME

Wilaya ya Tarime ina kilometa za mraba 1,791.504 kati ya eneo hilo kilometa za mraba 270 ni eneo la hifadhi ya mbuga ya Akiba ya Lamani (Game Reserve). Eneo linalotumika kwa shughuli za kilimo, ufugaji na makazi ya watu ni kilomita za mraba 1,521.504.
Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 1958, Wilaya ya Tarime wakati huo ilijulikana kama North Mara ilikuwa na watu 145,441. Sensa zilizofuatia zilionyesha kuwa mwaka 1967 ilikuwa na watu 188,536, mwaka 1978 ilikuwa na watu 253,010 mwaka 1988 watu 33,888, mwaka 2002 watu 490,731 kwa maoteo ya mwaka 2010 watu 359,032 kati ya hao, wanaume ni 170,450 na wanawake ni 188,582.
Wakazi wa Tarime.
Mboga mboga.
Biashara ya nafaka ikiendelea nje ya mashine ya kukoboa na kusagisha.
Nafaka kwaajili ya nguna.
"Ng'ombe dume akamuliwi maziwa"
Kama unaupungufu nguvu za kiume kamata namba hizo bangoni.
Mjini kati Tarime.
Kijiwe.
Vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Nyiboko iliyopo katika wilaya ya Serengeti vimeezuliwa mabati kupitia mvua iliyoambatana na upepo kunyesha mnamo mwishoni mwa mwaka jana ambapo hadi leo wanafunzi wa shule hii wanasoma katika hali ngumu kwenye madarasa haya.

Jua linawatandika mchana wakiwa kwenye masomo, mvua ikinyesha wanafunzi wanatawanyika.
Utoro umekithiri kwa wanafunzi na hata wengine kuacha kabisa shule kukwepa kadhia hizo.
Diwani wa kata hii anaishi Dar es salaam.  Zaidi nitawaletea full data na picha zaidi kupitia G. Sengo Blog.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Mkuu tujulishe na picha tuwekee ni shule niliyosoma.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.