ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 9, 2013

BASI TU BINADAMU MJANJA LAKINI NI SEHEMU YA WANYAMA.

WANYAMA ni viumbehai wasio mmea. Jina la kisanyasi ni animalia.
Hawapati chakula chao kupitia usanisinuru (nishati ya jua) lakini kutoka kwa viumbehai vingine ama wanyama wengine au mimea. Wanyama wanahitaji oksijeni kwa kupumua.
Wanyama walio wengi hutembea yaani hubadilisha mahali wanapokaa kwa hiyo wanahitaji milango ya maarifa.
Sayansi ya wanyama huitwa zoolojia.
Wala mimea huitwa herbivori na wala nyama huitwa karnivori. Kuna pia wanyama wanaoitwa omnivori yaani wanakula kila kitu ama mimea au wanyama wengine.
Aina za wanyama ni nyingi sana. Mara nyingi aina zao zinatofautishwa kama ni wanyama wenye seli nyingi (metazoa) au seli moja (protozoa) tu.
Kuna wanyama wanaoishi pekee yao, katika vikundi na jamii. Mfano wa wanyama wanaoishi pekee yao ni kifaru au nyoka. Wanajumuika kwa tendo la kuzaa pekee. Mfano wa wanyama wa jumuiya ni simba wanaokaa na kuvinda pamoja. Ishirikiano unasaidia kupata chakula bora. Mfano wa wanyama katika jamii ni nyuki na wadudu wengine.
Kibiolojia hata binadamu ni mnyama kimaumbile ahesabiwa kati ya mamalia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.