ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 9, 2013

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA YASHEREHEKEA MIAKA 52 YA UHURU BENDERA YAKE IKIPEPEA NUSU MLINGOTI.

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo ataongoza mamilioni ya Watanzania katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 tangu Tanganyika kupata uhuru ambayo baadaye iliungana na Zanzibar na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati hayo yakijiri itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kusherehekea uhuru wake huku bendera yake ikipepea nusu mlingoti kufuatia msiba mkubwa uliotokea wa kiongozi mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21 kiongozi wa kwanza mweusi nchini Afrika ya Kusini Nelson Mandela aliyefariki dunia mnamo tarehe 5 Desemba 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa hotuba ya salamu za rambirambi aliyoitoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa taifa la watu wa Afrika ya Kusini na Dunia, Jk alitangaza siku 3 za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba 2013 na kuagiza bendera zote kupepea nusu mlingoti.

Na sasa inatajwa kuwa siku moja zaidi imeongezwa (yaani leo tarehe 9 Desemba 2013) kwa ajili ya kuthamini mchango wa Mwamba huo wa Afrika ulio dondoka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.