ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 16, 2013

BONDIA AUMIA AKIJIANDAA NA MPAMBANO.

Enest Bujiku akisaini makubaliano ya mwisho kwa ajili ya mpambano wake na Shah Kasim.
Lusekelo Daudi akiwa tayari kumkabili mpinzani wake.

Moro Best
Shafii  Ramadhan.

BONDIA  AUMIA  AKIJIANDAA  NA  MPAMBANO


Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Shafii Ramdhan ameumia akiwa mazoezini  akijiandaa na pambano la tarehe 22 decemba pale Friends Corner hotel Manzese.
Ramadhan aliyekuwa acheze na Hassan Kiwale "Moro Best" alikutana na mkasa huo mazoezini kwake, taarifa hii iliripotiwa na kocha wa shafii ambae ni Jafari Ndame kwa Ibrahim Kamwe wa Bigright Promotion kuwa kutokana na hali hiyo Shafii hatoweza tena kucheza na Moro Best  na daktari pia hatoweza kucheza, na sasa imepangwa Hassan Kiwale `moro best` atacheza na Issa Omar NAMPEPECHE, kwa kuwa Issa Omar ni mkali kiasi Bigright Promotion imekubali kumuongeza kiasi cha pesa moro best kucheza pambano hilo. 
Moro best na  Issa Omar watacheza pambano hilo katika kuwasindikiza Japhet Kaseba  anaetetea ubingwa wake dhidi ya  Alibaba Ramadhan  ambae ni bingwa wa kanda ya kaskazini, pia kutakuwepo na pambano lingine la ubingwa kati ya Fadhili Awadh atakae minyana na Karage Suba. 
Wakati Mbaruku Heri na Mbabe mwenzake Lusekelo Daudi wanajaribu kumalizia kiporo chao kisichoisha kwani wameshacheza mara mbili katika ushindani mkubwa na mara zote wametoka sare mara hii wote wameahidi chochote na kitokee lazima pambano liwe na mshindi. 
Nae Adam yahaya [baby edo] atazipiga na Harman Richard, huku mkongwe Ernest Bujiku [tyson] atacheza na shah kasimu , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  Mbena Rajabu, nae  Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengela .
Pia siku hiyo kutakuwepo na lile pambano la mateke (kickboxing) la mtanzania anayeishi Canada Kareem Kutchi  na Mbongo Halisi Said Juma `tata boy`. Tayari kiwango Security ikisaidiana na jeshi la polisi wameahidi kutoa mchango mkubwa katika ulinzi na usalama wa watu wote watakaokuja katika  pambano hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.