ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 15, 2013

BREAKING NEWS: ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA CLEMENT MABINA AUAWA.

Marehemu Clement Mabina.
MWENYEKITI wa zamani wa chama cha mapinduzi(ccm) mkoa wa Mwanza Clement Mabina ambaye pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.

Tukio la kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Dk Antony Diallo lilitokea leo asubuhi katika eneo la kijiji cha Kanyama wilayani Magu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa tukio limetokea majira ya saa mbili asubuhi.

ODC Mkapa alikiri kutokea kwa tukio la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi wa eneo la kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake alikokuwa amekwenda kupanda miti.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema kuwa amepokea taarifa za kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa kuwa amesikitishwa sana na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.

Taarifa zaidi toka eneo la tukio la Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm alifika katika eneo hilo majira ya asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na wananchi.

Baada ya kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.

Baada ya majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kupoteza maisha.

Taarifa hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kabla ya kurejea chama cha mapinduzi(ccm) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya Kisesa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Malaki Lupondije.

Tupe maoni yako

18 comments:

  1. Mnakosea kusema bahati mbaya kumpiga mtu risasi, kama alitoa silaha na kuanza kuvyetua maana yake alijipanga kwa lolote. Msiwapotoshe watu, pia na yeye ameua hivyo ukiua kwa upanga nawe hivyohivyo. Wapo wengi wa aina yake wanatumia mabavu kuwanyang'anya watu wa chini haki zao hasa hawa CCM wanajiona kuwa wao ni miungu mtu.Hiyo ndo halali yao watu kama hawa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naunga mkono hoja. Viongozi waliochini ya mwavuli wa CCM wamekuwa wakitumia mabavu kudhurumu wananchi mali zao, hasa ardhi. Pia hayo mambo ya kuwatwanga watu risasi na kudai ni bahati mbaya,huu ni wendawazimu. Mtu ametoa silaha mfukoni na alikwenda nayo akijua kitakachotokea, na ndiyo kimetokea.

      Delete
  2. Watanzania tuishi kwa upendo na Amani aliyotupatia Mungu.

    ReplyDelete
  3. Fisadi Mabina katangulia,wengine mnaodhulumu wananchi mtamfuata huko kuzimu anakoungua moto.

    ReplyDelete
  4. Wanafiki wanaumia kifo cha mabina tu,wanadhani yule kijana aliyeuawa wa miaka 12 si chochote kwao,wasenge baridi nyie!

    ReplyDelete
  5. Kwann ajbu watu ovyo? kwann afyatue risas? kwann aende kupanda miti wakat shamba lna mgogoro? huu ni ubabe alpanga kufanya sasa kafaid

    ReplyDelete
  6. Tanzania ya leo si ya zamani viongozi mliopo madarakani musiitafute hasira ya wananchi masikini kwa kiburi kuwa mtalindana. kwa kuwa ninyi mmeshika mpini na masikini makali lolote mwaweza fanya kujipoza kwa machungu ya ndugu yenu. lakini mjue hata mtoto aliyeuliwa na Mabina ana thamani mbele za Mungu. KUMBUKA hiyo rangi ya kijani ina tatizo kumbuka Rais Nyerere hakuipendelea sana kuivaa alipokuwa na watanzania wa makabira vyama itikadi tofauti mikutanoni. jifunzeni.

    ReplyDelete
  7. YAMETIMIA YALIYOANDIKWA KUWA UKITAWALA KWA UPANGA UTAKUFA KWA UPANGA R.I.F MABINA

    ReplyDelete
  8. Ng'wagabona amakajashu!

    ReplyDelete
  9. Nina masikitiko kwani sikutegemea kama kiongozi mkubwa kwenye chama ,ambaye amewahi kukaa meza moja na mkuu wa nchi anawezakuishindwa namna ya kuwasiliana nawanchi wenye jazba,nahatua yenye afya ambayo inafaa kuchukuliwa ,AMANI KWANZA MENGINE BAADAYE hili liwefundisho kwetu kuwa elimu tuliyo nayo itusaidie kutafuta mahusiano mema na jamii,mali zinatafutawa,lakini maisha yakipotea basi. no more.

    ReplyDelete
  10. Hawa mafisadi wa CCM wamezoea kutumia mabavu kupora mali za wanyonge. Mfano mwingine ni Waziri mmoja (mwanamke) wa serikali ya awamu ya nne amepora mashamba ya wananchi eneo la Kibaoni-Kimwani Muleba na kuzungushia fensi eneo la kama hekta 400. Uporaji huo ulishirikisha matumizi mabaya ya madaraka aliyonayo kwa kutumia polisi kufukuza hadi kuwapiga wamiliki halali wa maeneo hayo na hakukuwa na fidia yeyote.
    Eee Mola,ulinyoosha mkono wako kwa fisadi Ditopile,leo fisadi Mabina,tunaomba kesho awe waziri huyu mwanamke ili liwe fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia hiyo. Ukizingatia kutoka barabara ya Kibaoni hadi ghuba ya Kabwinyola-Kimwani, ni eneo kubwa sana,hivyo ingependeza kuonyesha uzalendo kwa kuwarudishia ardhi wananchi aliowapora ardhi yao.

    ReplyDelete
  11. Don't think being politician is everything, pia watanzania acheni unafiki mi nadhani sheria ibadilike ukiuwa na wewe uuliwe maanake mambo ya kusema alikua kiongozi mkubwa kukaa meza moja na mkuu wa nchi is just nonsense hata hao wakuu wa nchi watapita na wasipojali na kuheshim waliowaweka kwenye huo ukuu lazima lazima watapoteza maisha tu kwani wamepoteza maisha ya wanyonge wengi sana ila wakipita wanafiki na wapuuzi wanawapigia makofi....

    ReplyDelete
  12. Daah...bado siamin et....

    ReplyDelete
  13. Jamani,mnaona rahisi kusema,na jinsi mnavyofikiri,huwezi kujua uharisia wa tukio na jambo lenyewe jinsi lilivyokuwa,yule ni binadamu, huenda hata wewe lingekuelemea tofauti na unavyojaji sasa hv.Hata hivyo unavyomhukumu,unajua nini kilichoko mbele yake na Muumba wake?Jihukumu kwanza wewe.Mola wasamehe hawa ndugu zetu waliltutangulia.Amina

    ReplyDelete
  14. Mie naomba waandishi, wanausalama na wanasiasa wasilipambe tukio hilo kwa kusema Mabina alipiga risasi juu kujaribu kuwatuliza wananchi wenyejaziba! Je, huyo mtoto alikuwa anafanyanini huko juu mpaka apatwe na mauti ya risasi za Mabina? Na kwanini aliondoka na Bastola tena na Shotgun kama vile anaenda kupambana na wanyama? Huyo dhamira yake ilikuwa ni kuua, alichokidhamiria kwa wana Kanyama ni bora kimeishia hapo maana walikuwa hawapumui!

    ReplyDelete
  15. Kwahiyo huyo mtoto alikuwa anawanga hewani? Semeni ukweli tu wananchi wamechoka na Ufisadi wa kila kitu hapa BONGO, nadhani karibu hawa mafisadi watahujumu hata hewa tunayoivuta. Hilo ni FUNDISHO, Kama huamini jifanye FISADI ujaribu uone!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. maoni yote hayana busara kwenye matukio makubwa kama haya. Achani uvivu wa kufikiri.

    ReplyDelete
  17. hili tukio lina ukubwa gani?? hebu acha uvivu wa kufikiri mwenyewe, watu mnapritendi mnapenda ukweli lakini ukikukuta unataka kubadilisha. Uhai wa mtu yeyote ni sawa hakuna cha mtu maarufu au mtu wa kawaida kama vp rudisheni basi uhai wa watu maarufu. ukweli ni kwamba busara ya kweli ni kusema ukweli na sio kubabaisha mara ikaenda mara ikarudi what the fuck?? kwa tukio kama hilo ni ngoma droo..

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.