Mwimbaji wa bendi ya Super Shine, Queen Salma akifungua pazia la burudani. |
Nuru Moshi wa Super Shine akitoa burudani. |
Waimbaji wa Super Shine wakiimba. |
Khadija Omar Kopa wa TOT akitoa burudani. |
…Akiviringisha kiuno chake. |
Mashabiki waliojitokeza kushuhudia onyesho hilo. |
Khadija Kopa akicheza na baadhi ya waimbaji wake. |
Ally J wa kundi la Five Star akipagawisha mashabiki. |
Maua Tego wa Five Star akiimba. |
Hashim Saidi wa Mashauzi akiwapagawisha mashabiki. |
Waimbaji wa Mashauzi wakiserebuka. |
Fatma Machupa wa Jahazi akiimba. |
Fatma Mahamud wa Jahazi naye akiimba. |
MC wa tamasha hilo, Khadija Shaibu ‘Dida’ (kushoto) akipozi na wenzake. Kulia ni msanii wa maigizo, Monalisa. |
Monalisa akiwa na shabiki wake. |
MC Dida akisherehesha. |
Mabaunsa wakilinda usalama wa mali na mashabiki. |
Dida (kushoto) akikabidhiwa keki na shabiki wake. |
Mtangazaji wa Times FM, Cliford Ndimbo, akiwa na mkewe. |
Dida akipozi na mumewe. |
Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live usiku wa kuamkia leo ulitikisika kutokana na kufurika mashabiki ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la Mitikisiko ya Pwani lililoandaliwa na Redio TIMES FM kwa udhamini wa Vodacom.
Katika onyesho hilo, bendi tano za miondoko ya taarab zilidondosha burudani ya nguvu ambayo iliwafanya mashabiki wa miondoko hiyo washindwe kutulia katika viti vyao.
Pazia la burudani hiyo lilifunguliwa na kundi la Super Shine ambao waliingia na staili ya ngoma ya Kimwera ambayo ilisababisha mashabiki kuwashangilia kwa nguvu.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/ GPL)
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/ GPL)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.