Vyumba vipatavyo SITA vya madarasa ya shule ya msingi Nyiboko iliyopo katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara vimeezuliwa mabati kupitia mvua iliyoambatana na upepo kunyesha mnamo mwishoni mwa mwaka jana ambapo hadi leo wanafunzi wa shule hiyo wanasoma katika hali ngumu kwenye madarasa haya.
Jua linawatandika mchana kutwa wakiwa kwenye masomo, mvua ikinyesha wanafunzi wanatawanyika na wengine wakijisitiri kwenye kingo za baadhi ya madarasa yaliyosalia na mabati. Utoro kwa wanafunzi umekithiri hali iliyo sababisha wanafunzi wengine kuacha kabisa shule kukwepa kadhia hizo ikiwemo ya wanafunzi kukaa chini kwa kukosa kabisa madawati.
Akina dada wanao ikimbia shule hiyo wakikatisha masomo wanageukia biashara ya ukahaba wakiwa na changamoto ya kukosa elimu na kutojitambua na hata maamuzi yao ni ya kukurupuka ambayo mwisho wa siku yanasababisha ongezeko la ukatili wa kijinsia.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.