Mangu ameyasema hayo katika uzinduzi wa siku 16 za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake uliofanyika juzi katika viwanja vya line polisi Mabatini jijini Mwanza.
“Uwepo wa matukio hayo unaleta haja ya walio katika nafasi kusimama na kuzuia vitendo vya ukatili” alisema kamanda Mangu
Mpaka sasa mkoani Mwanza matukio ya mauaji ya kishirikina yamefikia 40 na watu 44 wakipoteza maisha katika matukio hayo wanawake wakiwa ni 34 na wanaume 10 tu. Huku watuhumiwa 133 wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Masele amesema kampeni hiyo ya siku 16 inalenga kuamsha ari kwa watanzania kupambana na ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake na kauli mbiu ya kampeni hiyo ni “Funguka ! Tumia mamlaka yako, zuia ukatili wa kijinsia, kuboresha afya ya jamii.
Bw. Masele amebainisha kuwa kukosekana kwa sheria maalumu inayohusika na ukatili wa kijinsia, mitazamo hasi ya jamii dhidi ya wanawake, ukosefu wa huduma bora za afya na vitisho kwa wahanga wa ukatili ni baadhi ya changamoto zinazo wakabili katika harakati za kupambana na ukatili wa kijinsia.
Pia Diwani wa kata ya Mbugani Bw. Hashim Hassan Kijuu ameitaka jamii kushirikana katika ngazi zote toka familia, mtaa mpaka taifa kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Shirika la KIVULINI limekuwa likendesha harakati za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na siku ya Novemba 25 ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake duniani.
Awali kabla ya maadhimisho yaliyanyika maandamoano kutoka viwanja vya wa Ghand Hall hadi eneo la tukio uwanja wa Mabatini jijini Mwanza. |
Ngoma asilia. |
Burudani kama sehemu ya kunakshi kusanyiko la maadhinisho hayo. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.