ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 4, 2013

GLOBAL EDUCATION LINK YAZINDUA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NJE YA NCHI

Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje    ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu.  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba akiongea machache katika uzinduzi wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa ndiyo uzinduzi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOAH akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wazazi waliohudumiwa na taasisi ya Global Education Link wakitoa ushuhuda wao jinsi watoto wao walivyowezeshwa kutafutiwa nafasi za masomo kwa vyuo vya nje ya nchi bila usumbufu kwa vyuo vinavyotambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. Ambapo wazazi hao walitoa rai yao kwa wazazi wengine kuendelea kuiunga mkono GEL ili isonge mbele zaidi kwa vile inafanya kazi zake kiuhakika bila ya kudanganya.
Waliongeza kuwa kwa sasa wanafunzi wengi wamekuwa na moyo wa kusoma nje ila kuna baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa yakiwadanganya na kujikuta wakidondokea kwenye vyuo ambavyo havitambuliki mwisho wake kuishia kupoteza hela na muda. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaama.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (katikati) akizindua. Pembeni toka kulia ni Wafanyakazi wa GEL, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOA, Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa pamoja na Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba.
Hiki ndicho kilichozinduliwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.