ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 4, 2013

BODI YA PAMBA NA UMOJA WA ULAYA (EU) ZAANZA KUWAWEZESHA WAKULIMA KULIMA PAMBA BORA.

Mratibu wa Mradi wa Kilimo cha zao la Pamba na Biashara wa Bodi ya Pamba nchini TCB Renatus Luneja akikabidhi baiskeli kwa wakulima 30 kutoka vijiji  13 vya wilaya ya Maswa ambao ni wakulima wawezeshaji ili kusaidia kutoa elimu na mafunzo ya kilimo bora cha pamba ikiwa ni msaada ulifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa wilaya tatu za Maswa, Meatu na Bariadi.
Baiskeli zilizotolewa.
Sehemu ya wakulima wawezeshaji 35 kutoka vijiji 20 wakiwa na picha ya pamoja na mratibu wa mradi huo Renatus Luneja wakati alipowagawia baiskeli hizo Wilayani Bariadi hivi karibuni
Katibu tawala wa Wilaya ya Maswa (DAS) Chale Ndaki  akiwa na Mratibu wa Mradi Renatus Luneja (anayesaini kitabu), kulia ni Mhasibu wa Mradi huo Felix Ikongo walipofika ofisini kwake baada ya kukabidhi baiskeli kwa wakulima wawezeshaji.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa kiwanda cha Nsagari, Emanuel Gungu ambaye pia ni mnunuzi wa Pamba, nyuma ni Katibu tawala wa wilaya hiyo Rutaiwa.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima akikabidhi baiskeli kwa mmoja kati ya wakulima.

Picha ya pamoja.
Wakulima wakikagua baiskeli zao mara baada ya kukabidhiwa.
Shughuli imemalizika sasa twenzetu kwenye majukumu.
Haoooo...
JUMUIYA ya Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba imeaanza kuchukua hatua ya uboreshaji zao la pamba kwa kufadhili mradi wa kilimo na biashara (TASP II) sehemu ya pili kwa kutoa usafiri wa Baiskeli 100 kwa wakulima wawezeshaji 100 katika Wilaya tatu za Mkoa wa Simiyu.

Wakulima wa zao la Pamba katika vijiji 48 vya  Wilaya ya Maswa, Mneatu  na Bariadi Mkoani humo  wamenufaika na mradi huo  kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao la Pamba kutoka Kilo 300 kwa Ekari hadi kufikia kilo 1,500 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo baada ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuanza kufadhili zao la Pamba katika Wilaya hizo  kwa majaribio.

Hatua hiyo inatokana na Bodi ya Pamba kugawa baiskeli 35 kwa wakulima wawezeshaji 35  kutoka vijiji 15 vya Wilaya ya Meatu , wakulima 30 kutoka vijiji 13 vya Wilaya ya Maswa na wakulima 35 kutoka vijiji 20 vya Wilaya ya Bariadi ambazo zimegarimu zaidi ya shilingi milioni 15 ambapo watatumia kuwafuata wakulima na kuwasaidia kuwapatia elimu na mafunzo ya kanuni bora za kilimo.

Akizungumza wakati wa kukabizi Baiskeli hizo katia Wilaya hizo Mratibu wa Mpango wa kusaidia Kilimo na Biashara awamu ya pili (TASP II) katika Mkoa wa Simiyu Renatus Luneja amesema kwamba lengo ni kusaidia kuongeza mapato ya mkulima mdogo wa zao la pamba na kusaidia kuimarisha ubora ili kuwa na uhakika wa soko la pamba ndani ya nchi na nje ikiwa pia kilimo chenye tija kumuinua mkulima na kurudisha heshima ya Pamba Dhahabu Nyeupe kwenye soko.

“Tumeanza na hawa wakulima wawezeshaji wapatao 100 kutoka Wilaya hizi tatu kunako tekeleza mradi huu kwa majaribi kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2015 kwa kutoa baiskeli aina ya PHONEX kwa wakulima hawa kusaidia kutoa elimu na mafunzo kwa wenzao ili wafuate kanuni bora za kilimo cha zao la pamba ili kufikia malengo ya kufika katika uzalishaji wa kilo 1,500 kwa ekali ifikapo 2015” alisema Mratibu huyo.

Luneja alieleza kuwa utendaji makini wa wakulima wawezeshaji katika maeneo mbimbali unatakiwa kuwa wenye tija ili kuwezesha wakulima kutekeleza kwa vitendo Kilimo na Biashara ya Pamba Tanzania sehemu ya pili kwenye Wilaya ambazo zitakuwa za majaribio kupi vikundi vya wakulima kabla ya kuendelea kwenye maeneo mengine za Kanda ya Magharibi zenye kujishughulisha.

“Vitendea kazi hivi tulivyowapatia ambavyo vimetolewa kwa ufadhili wa EU na kugarimu zaidi ya milioni 15 hakika mvitumie kuwahamasisha wakulima mikwa wawezeshaji kwa kuleta tija kwao na kupatikana pamba nyeupe yenye ubora na kuwezesha soko la ukakika ”alisisitiza Luneja.

 Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu  Chele Ndaki ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Meatu amewataka wakulima hao kutumia vyema usafiri huo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuhakikisha wanawawafikia wakulima wenzao kuwapatia maarifa ya kutumia kanuni bora kama wanazotumia wao ili kuwa na kilimo cha tija na kuwaongezea kipato.

Ndaki pia ameupongeza Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba nchini kuthamini na kurejesha matumaini kwa wakulima kwa kuanza kuchukua hatua za kuokoa zao la pamba na kuhakikisha ubora wa pamba dhabu nyeupe unarudi na kuwa na uhakika wa soko la ndani na mataifa ya nje ili kureta kipato kwa mkulima na ubora.


“Wakulima wawezeshaji watawasaidia wakulima wadogo kwa kuwaelimisha na kuhamasisha vikundi kuanza kutenga maeneo ya kilimo ikiwa ni mashamba darasa kila Kata kwa lengo la kuwapatia mbinu na mafunzo ya kitaalamu ya kilimo cha zao la Pamba huku pia wawekezaji wa kilimo cha zao hilo nao wakianzisha mashamba darasa kwenye Kata kupitia kwa wakulima wa vikundi watakaoingia navyo mkataba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.