ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 4, 2013

ASILIMIA KUBWA YA MIGODI KANDA YA ZIWA INACHANGIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA


Tarehe 25 Agosti – 18 Sept. 2013, Baraza limekagua shughuli za utunzaji mazingira kwenye migodi, hususani migodi mikubwa iliyoko Kanda ya Ziwa.
Lengo la ukakaguzi ilikuwa nikuangalia jinsi miradi hiyo inakidhi matakwa ya kisheria juu ya utunzaji na usimamizi wa mazingira migodini
Ukaguzi ulihusisha Migodi ifuatayo:
}  Resollute Mining Project
}  Buzwagi Mining Project
}  Bulyanhulu Mining Project
}  Tulawaka Mining Project
}  North Mara Mining project
}  Kabanga Nickel project
}  Geita Gold Mine Project
}  El-Hillal Diamond Mine Project
}  Williamson Diamond Mine Project
Ukitaka kujua athari za kemikali tizama mimea iliyo ndani ya haya maji imekauka ile hali iko ndani ya maji...
Baadhi ya athari zitokanazo na uchimbaji wa madini ni:
}  -uharibifu wa ardhi
}  -uchafuzi wa maji na hewa
}  -Upoteaji wa Bioanuai
}  -Uharibifu wa mandhari
Mapipa yenye kemikali zinazovuja ardhini na kuathiri rutuba ya ardhi na kuua mimea.
Mfereji unaotiririsha oil chafu inayozama ardhini na kuathiri rutuba ya ardhi hatimaye inaua kabisa mimea na wadudu wa asili waishio ardhini.
Vitengo vingi vya uzalishaji hususani vile vinavyotumia kemikali havina udhibiti wa kuwa na mabwawa maalum yanayopokea kemikali hizo wala mifereji yenye kingizo za vyuma, plastiki au mifereji ya sementiinayodhibiti kemikali kuzama ardhini ambako huenda kuathiri udongo.
Mfereji unaotiririsha kemikali zinazozama ardhini na kuathiri rutuba ya ardhi na kuua mimea.
Utupaji hovyo wa taka ngumu uliokithiri kwenye migodi.
 Ukaguzi wa shughuli za mazingira umeonyesha mapungufu katika maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
- Utupaji wa taka ngumu
-         Kudhibiti majitaka yasiyosafishwa
-         Udhibiti wa oili na kemikali
-Utunzaji na usimamizi wa Mabwawa ya kemikali (Tailing dams)
-Utunzaji na udhibiti wa kemikali
Haakuna udhibiti wa maji yenye kemikali ambayo hayajasafishwa.
Uharibifu wa ardhi migodini kupitia vyuma chakavu, kemikali na taka ngumu.
Vyanzo vingi vya maji vimeathiriwa na kemikali zinazomiminika toka migodini.
Madawa na kemikali hayahifadhiwi kwenye maghala yanayostahili.

SERA, MIKAKATI, USIMAMIZI NA UDHIBITI
Uchimbaji wa madini endelevu ni muhimu ili kulinda mazingira na kuleta maendeleo endelevu.
Ni muhimu kutambua na kutumia njia bora za utunzaji mazingira katika uchimbaji madini
Serikali imechukua juhudi mbalimbali za kufikia uchimbaji endelevu. Mwaka 1997 Serikali ilitunga Sera ya Mazingira ya Taifa mwaka 1997. 

Sera hii inasisitiza umuhimu wa kuhuisha masuala ya mazingira katika sera nyingine na programu mbalimbali ili kufikia uchimbaji madini ulio endelevu na shirikishi.

Sera ya Mazingira inajumuisha majukumu ya kisekta kama sekta ya madini katika kuhakikisha masuala ya mazingira yanaaangaliwa na kutekelezwa. Sera inabainisha kuanzishwa kwa Sheria ya Mazingira ambayo inaainisha majukumu ya taasisi na wadau wengine katika kutunza mazingira. Sheria ya Mazingira (Sura 191) ya mwaka 2004 imeweka majukumu ya kisheria ya kutunza mazingira katika shughuli za uchimbaji madini.

TAMKO LA BARAZA
}  Baraza linayataka makampuni yote ya migodi kuzingatia taratibu zote za usimamizi wa mazingira kama zilivyoainishwa katika MIPANGO YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA  - EMPs
}  Kusitisha shughuli zote zinazokusudia au kuashiria kuharibu Mazingira
}  Kutekeleza maelekezo yote yaliyoanishwa kwenye barua za makatazo (Environmental orders)
}  Baraza halitendelea kuvumilia uharibifu wa mazingira kuendelea kwa manufaa ya umma na Taifa kwa ujumla.
}  Baraza pia liliendelea kukuza ufahamu kuhusu umuhimu wa kupunguza athari za shughuli za maendeleo katika mazingira na afya za viumbe hai na kuleta maendeleo endelevu.
}  Msisitizo: Katika suala la utunzaji wa mazingira na udhibiti wa uchafu, kinga ni bora kuliko tiba hapo baadae.

}  Uhifadhi na udhibiti wa kemikali ni jambo la muhimu sana 

UMUHIMU WA SEKTA YA MADINI.
}  Sekta ya madini hasa uchimbaji mkubwa hapa Tanzania ni sekta inayokua kwa kasi na inayochangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi.
}  Mwaka 2005/2006, sekta ya madini ilichangia karibia asilimia 3.5 ya pato la taifa na ilifikia asilimia 42.4 ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi kwa mwaka huo.
}  Dira ya sekta ya madini kuelekea 2025 inalenga kuchangia asilimia 10 ya pato la Taifa.

}  Shughuli za uchimbaji madini husababisha uharibifu wa mazingira. 

Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepewa mamlaka ya kusimamia shughuli za utunzaji wa mazingira nchini chini ya sheria No. 20 ya Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira (EMA) ya mwaka 2004 ibara ya 17 (1) na  25

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.