ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 12, 2013

DKT. SENGODO MVUNGI AFARIKI DUNIA.

Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengodo Mvungi(Pichani) amefariki katika hospitali ya MillPark huko Afrika ya kusini alikokuwa akipata matibabu.

Dk. Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

: Kwa mujibu wa Hussein Bashe Bashe "Dr Sengondo Mvungi Is No More,Taarifa zilizonifikia kutoka Milpark Hospital Ndg. yetu Mvungi Amefariki,Mnamo Majira ya Saa Tisa na Nusu.Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.

Wahalifu wamekatisha Uhai wake wakati akifanya Jukumu zito kwa Ajili ya Taifa letu.Jambo hili linaumiza sana Mungu Atalipia Uhalifu huu. poleni Tume ya Katiba,Poleni Familia,Poleni NCCR."Dr Sengondo Mvungi Is No More,Taarifa zilizonifikia kutoka Milpark Hospital Ndg yetu Mvungi Amefariki,Mnamo Majira ya Saa Tisa na Nusu.Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.
 KWA HABARI ZAIDI ENDELEA KUFUATILIA VYOMBO VYA HABARI...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.