ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 29, 2013

RAN IT SOLUTIONS (EA) LTD YABORESHA MAABARA, HUDUMA ZA MAJI NA KUKARABATI NYUMBA ZA WAALIMU SHULE YA SEKONDARI MAGU

Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD,  Lugumi Enterprises LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi wake bw. Said Lugumi, akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Computer kwa ajili ya matumizi ya shule ya sekondari Magu katika Mahafari ya 24 ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne 2013 yaliyofanyika shuleni hapo.
SIKILIZA KILICHOFANYIKA KWA KUBOFYA PLAY.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule akiinyanyua juu Computer aliyokabidhiwa na Meneja wa Ran IT Solutions (EA) LTD, Lugumi Enterprises LTD na KZ Secury, Eligod Justine Sangawe  kwa ajili ya matumizi ya shule ya sekondari Magu katika Mahafari ya 24 ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne 2013 yaliyofanyika shuleni hapo huku wadau wengine wakifurahia tukio hilo.

Pia  kampuni ya Ran IT Solutions EA Limited, Lugumi Enterprises LTD na KZ Secury imekarabati na kukabidhi baadhi ya vifaaa vya maabara ikiwemo kuwapatia gesi na kuboresha mfumo wa maji wa maabara ya shule ya sekondari Magu.
Meneja wa Ran IT Solutions (EA) LTD, Lugumi Enterprises LTD na KZ Secury  Eligod Justine Sangawe (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kwa moja kati ya vitedea kazi vya maabara alivyokabidhi kwa Shule ya Sekondari Magu.
Hii ndiyo pump ya maji ya kutumia mkono ambayo ilikuwa ikitumika awali ambapo sasa kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD, Lugumi Enterprises LTD na KZ Secury imekabidhi pump ya kisasa ya inayotumia umeme ili kurahisisha utendaji kazi na huduma za shule.
Meza kuu.
Moja kati ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na
-Upungufu wa walimu hasa baada ya baadhi ya walimu wa shule hiyo kwenda kujiendeleza masomo ya elimu ya juu.
-Upungufu wa vitabu vya kiada na rejea.
-Upungufu wa matundu ya vyoo nane vya wavulana na vitano vya wasichana.
-Ukosefu wa rasilimali fedha kwaajili ya kukamilisha nyumba moja ya walimu ambayo mpaka sasa tayari imeezekwa lakini ikihitaji hatua ya ukamilishaji wa madirisha, milango, sakafu, vyoo, rangi, jiko, stoo, bafu mfumo wa maji na umeme ambapo Kampuni ya Ran IT Solution Limited (EA) LTD, Lugumi Enterprises LTD na KZ Secury imeahidi kumalizia nyumba hizo za waalimu.

Aidha Run IT Solutions (EA) Limited, Lugumi Enterprises LTD na KZ Secury imeahidi kuweka uzio kwa moja ya maeneo ya shule hiyo ili kudhibiti uvamizi wa mipaka ya shule.
Picha ya Pamoja na Maskauti wa Shule.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.