ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 29, 2013

WAKAMATWA NA KIGANJA CHA BINADAMU WAKIUZA KWA TSH 100 MILIONI

TAHADHARI KWA PICHA ZIFUATAZO KWANI ZINATISHA
Kiganja cha binadamu
WAGANGA wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja, wamenaswa jijini Mwanza, wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu.

Watuhumiwa hao waalikamatwa jana mchana majira ya saa 9 katika eneo la Ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na hatimaye kufanikiwa.
Kiganja hicho kilihifadhiwa ndani ya chungu.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo, akitihibitisha tukio hilo, alisema kwamba mkono huo uliokuwa umewekwaa kwenye begi na ambamo ulikuwa umefungwa kwenye kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye kalatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.

Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.

Alisema kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia wanunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo wangezihitaji.
 “Taarifa hizi ni za awali maana tukio lenyewe bado ni bichi kabisa na limetokea muda mfupi uliopita hivyo taarifa zaidi tutazitoa baada ya kukukamilisha upelelezi wetu ikiwa pamoja na kuwakamata watuhumiwa na kubaini binaadamu aliyeuawa na kukatwa baadhi ya viungo ambavyo waganga hao walidai wanaweza kuvipata.” Alieleza.

 Alieleza akwamba, kwa mujibu wa makubaliano hayo, wauzaji hao walkitaka kupewa sh milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
Ni unyama gani huu?
Ulinzi uliimarishwa katika eneo hili kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa.
Kamanda Konyo pamoja na kuwapongeza wananchi waliotoa taarifa zilizofanikisha mtego huo, alisema jeshi lake liko katika harakati za kupambana na mauaji na uhalifu wa kila aambapo tayari kikosi kazi kiko katika wilaya ya Magu kikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kinawatia mbaroni watu wanaojihusisha na uhalifu na mauaji.

Wananchi wakiwa katika hali ya kutafakari juu ya tukio hilo la kusisimua.
Bado ni mshangao kwa kila aliyefika eneo hili la kituo cha polisi Air Port Mwanza.
Watuhumiwa wakiwa na kiganja hicho cha binadamu.
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza wakiwaongoza watuhumiwa kuelekea eneo la usalama kwaajili ya mahojiano zaidi.
Wananchi na wafanyakazi wa Airport Mwanza wakiwa ma maswali juu ya sakata hilo.
Mara baada ya watuhumiwa hao kuondoshwa toka katika kituo cha polisi Airport Mwanza walifikishwa kituo cha polisi Kirumba kwaajili ya hatua nyingine za kisheria.
Kitupo cha polisi Kirumba jijini Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.