Bingwa wa Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Blantyre Malawi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya medali ya zahabu mwishoni mwa wiki. |
MCHEZAJI
watimuya Safari Pool Taifa, Patrick
Nyangusi ameibuka Bingwa wa Afrika katika mashindano ya mchezaji mmoja mmoja (singles)
wanaume yaliyo jumuisha timu sabakuto kakatika Nchi sita za Afrika.
Patrick
Nyangusi aliupata ubingwa huo kwa kumfunga mchezaji bora wa Afrika Kusini, Vishen Jagdev
6- 4, katika mchezo ambao ulisisimua wapenzi na mashabiki wengi wa mchezo huo uliofanyika katika ukumbi wa kisasa wa Roben
Complex jijini Blantyre.
Nyangusi kwa ubingwa huo aliza wadiwa medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili alichukua mpinzani
wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini ambaye alizawadiwa Medali ya Silver
wakati mshindi wa tatu ni Moses Mofya kutoka Zambia ambaye alimfunga mchezaji wa
Tanzania, Omary Akida, 5-3 na hivyo Moses Mofya kuzawadiwa Medali ya Fedha na nafasi ya nne ilichukuliwa na mchezaji kutoka
Tanzania, Omary Akida.
Upande wa timu zilizowakilisha Nchi,
Zambia waliibuka mabingwa katika mchezo ambao uliendeshwa kwa mfumo wa ligi ambapo Zambia
waliongoza kwa pointi 14.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na timu kutoka Nchi ya Afrika Kusini kwa pointi
12, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Nchi ya Tanzania ambao walipata pointi 9,
wakati nafasi ya nne ilibaki kwa wenyeji Malawi ambao walipata pointi 4.
Akizungumza Mkurugenzi wa mashindano ya
AAPA (All Africa Pool Associations), Rick Schoenlank,
alizipongeza Nchi zote zilizo shiriki mashindano hayo, pili aliwapongeza waandaaji wa mashindano kwa maandalizi mazuri na mwisho aliipongeza
Tanzania kwa kutoa bingwa wa Singles kwa mwaka 2013.
Nae mgeni rasmi aliyefunga mashinndano hayo,
Mjumbe wa Baraza la Michezo la Nchini Malawi, Sharaf Pinto,
kwa niaba ya Waziri wa michezo wa Malawi, aliipongeza pia Tanzania kwa kutoa bingwa
Singles na kuwaomba Tanzania kuwa karibu na wachezaji wa Malawi
ili kubadilishana uzoefu na udugu pia kwa kutembeleana na kucheza mechi za kirafiki.
Lakini pia aliwapongeza
Zambia kwa kutwaa ubingwa wa timu na vilevile aliwapongeza Malawi kwa nafasi waliyopata simbaya sana,
ni nafasi ambayo inawafanya wajiandae vyema kwa mashindano yajayo.
Mwisho aliwapongeza kila Nchi kwa kuleta uwakilishi na kuwatakia
safari njema ya kurejea Nchini salama mpaka mashindano mengine mwakani.
Mashindano ya mwaka huu yalijumuisha Nchi takribani
6, ambazo ni Afrika Kusini, Zambia, Tanzania, Lesotho, Namibia na wenyeji Malawi 1 na
Malawi 2.
Timu ya
Safari Pool ililiyo kwenda Malawi ina jumla ya wachezaji 8, ambaoni Mohamed Idd,
Patrick Nyangusi Festo Yohana , Mereczedec Amadeus, Omary Akida, Abdalah Hussen, Godfrey Swain na Nahodha Charles Vernas na viongozi watatu ambao ni Meneja wa timu
Nabil Hiza, Katibu wa chama cha pool Taifa, Amos Kafwinga na Makamu Mwenyekiti, Fred
Mush.
Mashindano ya
AAPA mwakani yanatarajiwa kufanyika Tanzania jijini Dar esSaalaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.