Silaha zilizokamatwa. |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi. |
Akizungumza jana na mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi alisema kuwa opresheni hiyo ilitokana na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya tano za Mkoa huo na kwenye maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya Uwindaji kwa kipindi cha mwaka moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012.
Silaha zilizokamatwa za kisasa na za kienyeji. |
Kamanda Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na magazine 28 zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa na risasi zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa Hollo Mabuga (28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13 zilisalimishwa kwa hihali na baadhi ya watu waliokuwa wakizimiliki kinyume na sharia,Short-Gun saba, Gobole 17 na SAR moja.
Shehena ya risasi zilizo kamatwa. |
“Tumeweza pia
kumkamata mtuhumiwa hatari wa matukio ya uhalifu ambaye hivi karibuni aliachiwa
kutoka Gerezani lakini tukapata taarifa za raia wema kuwa amekuwa akijihusisha
na ujangiri na ujambazi ambaye ni Masanja Sumuni, tukaweka mtego na kufanikiwa
kumkamata akiwa na SMG moja na risasi 96 huku mke wake Hollo Mabuga akikutwa
pia na silaha” alisema.
Silaha za zilizotengenezwa kienyeji. |
Kufatia
operesheni hiyo Jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wane
katika maeneo ya Wilaya ya meatu huku zaidi ya watu kumi waliokuwa
wakijihusisha na ujangiri wakikutwa na nyara za serikali ikiwa niza wanyama
waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mapori ya Akiba katika Wilaya
za Meatu, Maswa na Itilima.
“Tumeunda kikosi
kazi ambacho pia kinaendelea na operesheni ya kuwakamata wafugaji na mifugo yao
ambao wamekuwa wakichungia mifugo ndani ya eneo la Hifadhi ya Serengeti ambapo
zaidi ya ng’ombe wengi walikamatwa na kutozwa faini ambapo zaidi ya shilingi
milioni 180 zilipatikana huku watu wanaoendesha vitendo vya ujangiri wakiuwa
tembo na wamyama na kuuza kwa wananchi wa maeneo ya jirani” alisema Kamanda.
Kamanda Msangi
amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za siri
zitakazowawezesha kuwakamata wahalifu na wahamiaji haramu katika maeneo yote ya
Wilaya za Meatu, Maswa, Bariadi, Itilima na Busega huku makakati wa kuanzisha
vikosi kazi kila tarafa ukiwa mbioni kukamilika ili kuimalisha ulinzi kwa
wananchi na mali zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.