ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 3, 2013

RAIS KIKWETE ZIARANI MWANZA

 RAIS, Dkt Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuanaanza ziara ya kiserikali ya siku nane Mkoani Mwanza, ambapo atakagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, iliyotekelezwa na serikali ikiwa ni utekelezwaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM .

Rais ambaye atawasili jijini hapa kesho asubuhi  asubuhi, baadaye ataelekea nchini Uganda kukutana na Rais wa wan chi hiyo, Yoweri Mseven, kabla ya kurejea  jijini Mwanza Alhamisi kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, Rais Dkt Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa wa Mwanza kujionea shughuli za maendeleo, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Injinia Ndikilo alizitaja shughuli hizo kuwa ni miradi ya Nishati ya Umeme wa Millennium Challenge Cooperation (MCC) unaofadhiliw na serikali ya Marekani uliotekelezwa katika wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Sengerema ambapo utazinduliwa katika Kijiji cha Bukokwa.


Mkuu wa Mkoa alifafanua kuwa, katika sekta ya afya, Dk Kikwete atafungua jengo la Zahanati ya Lugeye wilayani Magu, Maabara ya Hospitali ya wilaya ya Ukerewe na kuzindua X-ray mbili ikiwemo kubwa ya kisasa iliyotolewa na Denmark kwa ufadhili wa  Mbunge wa jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga.

Akiwa Misungwi katika sekta ya Afya atazindua pia E-xray ndogo  iliyonunuliwa na Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwa ajili ya Hospitali ya Mitindo ya wilaya hiyo na kufungua Shule ya Msingi ya Kisasa, Ntulya iliyojengwa na NGO ya Afrian School House ya Marekani kupitia Mbunge huyo.

Miradi mingine ni ya Ulinzi na Usalama ambapo atafungua Kituo kipya cha Polisi Nyakato Jijini hapa, mradi wa maji wa Katunguru Wilayani Sengerema, uwanja wa ndani wa michezo Malya Wilayani Kwimba na kuweka jiwe la Msingi katika Kanisa la Kisabato Pasiansi Wilayani Ilemela.

Wakati wa ziara hiyo katika maeneo atakayotembelea Rais, atazungumza na wananchi hivyo injinia Ndikilo ametoa  natoa wito kwao kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza, hii ni fursa ya pekee kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujionea shughuli za maendeleo yao zilizvyotekelezwa na serikali yetu kama utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha kuanzia 2010 hadi 2015 nchini kote.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.