Mbaspo yatoa onyo Airtel Rising Stars
· Yailarua Mbeya Sekondari 6-0
Timu ya Mbaspo Academy ilifanya mauaji juzi Jumanne kwa kubamiza bila huruma timu ya Mbeya Sekondari 6-0 katika mashindano yanayoendelea ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa. Mechi hiyo ilichezwa kwenye kiwanja cha Magereza mkoani Mbeya.
Washindi walifungua kitabu chao cha magoli katika dakika ya sita kupitia kwa mshambuliaji wao mahili Jackson Mwaibale aliyefunga magoli manne peke yake. Mshambuliaji huyo kinda aliifungikia tena timu yake magoli matatu katika dakika za 16, 20 na 74. Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya waliokuja kushangilia timu yao walijikuta kwenye hali ya kukata tamaa baada ya timu yao kuwanyong’onyesha na wapinzani wao Mbaspo.
Peter Noah, mshambuliaji mwingine hatari wa timu ya Mbaspo, aliifungia tena timu yake katika dakika ya 30. Alikua ni yeye tena katika dakika ya 68 alipoitimisha kalamu ya magoli baada ya kuwapita walinzi wa Mbeya Sekondari na kumuacha golikipa akiduwaa baada mpira kutinga wavuni.
Kwa upande mwingine timu ya Faru Boys football walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wapinzania wao Mapambano katika mechi ya ufunguzi ya ARS, katika mkoa wa Temeke uliofanyika katika uwanja wa Twalipo jumanne jioni jijini Dar es Salaam.
Timu zote zilianza mchezo kwa kasi na babada ya kosa kosa za hapa na pale hatimaye Yohana Joseph ilifanikiwa kuitoa kimasomaso timu yake alipounganisha krosi kutoka upande wa kushoto ambayo iliingia moja kwa moja wavuni. Goli hili lilipokelewa kwa furaha na washabiki wa Faru.
Mchezo mwingine wa Another Airtel Rising Stars, mkoa wa Ilala, ilichezwa kwenye kiwanja cha soka cha shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa ambapo timu ya Amana Shooting ilishinda 2-0 dhidi ya Msimamo Youth Academy. Magoli hayo yalipatikana kupitia kwa Isiaka Mohamed dakika ya 22 na Ally Shaban dakika ya 68.
Mkoa wa Mwanza ulitarajia kuzindua mechi zake za ARS ngazi ya mkoa leo, Juni 26 wakati Morogoro na Mbeya walitarajiwa kuendeleza na mechi za mashindano hayo leo, Juni 26, 2013.
Wakati huo huo, mkoa wa kisoka wa Kinondoni umetangaza kombaini yao ya wachezaji 15 watakaowakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yatakayofanyika wenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 7.
Wachezaji hao ni Hamza Mohamed, Hamza Abdallah, Twalib Athuman, Fred Bakari, Hazzad Jumanne, Salim James, Abubakary Mohamed, Willy Kalolo, Didas Proches, Mustafa Yusuf, Rashid Khalifan, James Msuva, Isiaka Lukana, Ally Amin na Shabani Idd.
Ends…
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.